WAKAZI WA BIHARAMULO KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA DOLA MIL.55.1 KUTOKA HUNGARY - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, April 2, 2026

WAKAZI WA BIHARAMULO KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA DOLA MIL.55.1 KUTOKA HUNGARY


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akimshukuru Balozi Mteule wa Hungary nchini Tanzania, Mhe. Katalin Nyirati kwa kufanikisha kusainiwa kwa Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 55.1 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Biharamulo Mkoani Kagera, hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akisaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 55.1 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Biharamulo Mkoani Kagera, hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akimkabidhi zawadi Balozi Mteule wa Hungary nchini, Mhe. Katalin Nyirati, baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 55.1 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Biharamulo Mkoani Kagera, hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akiteta jambo na Balozi Mteule wa Hungary nchini Tanzani, Mhe. Katalin Nyirati, baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika jijini Dodoma.

Balozi Mteule wa Hungary nchini Tanzani, Mhe. Katalin Nyirati, akitoa ahadi ya kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika nyanja za maendeleo baada ya kusainiwa kwa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani Milioni 55.1 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji Biharamulo Mkoani Kagera, hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (wa nne kushoto), akiongoza kikao kati yake na Balozi Mteule wa Hungary nchini Tanzania, Mhe. Katalin Nyirati, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi, Mwajuma Waziri, akiishukuru Hungary kwa kutoa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani Milioni 55.1 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji Biharamulo Mkoani Kagera, hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi, Mwajuma Waziri, akiteta jambo na Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bw. Rishe Bade baada ya kusainiwa kwa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani Milioni 55.1 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji Biharamulo Mkoani Kagera, hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, katikati ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Bw. Melckzedeck Mbise.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Balozi Mteule wa Hungary nchini Tanzania, Mhe. Katalin Nyirati na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi, Mwajuma Waziri, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na Hungary baada ya kusainiwa kwa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani Milioni 55.1 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji Biharamulo Mkoani Kagera, hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha)


Na. Peter Haule na Josephine Majura, WF, Dodoma


Serikali ya Tanzania na Hungary zimesaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 55.1 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Biharamulo Mkoani Kagera.

Mkataba huo umesainiwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania akishuhudiwa na Balozi Mteule wa Hungary nchini, Mhe. Katalin Nyirati.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa Mkataba huo Dkt. Mwamba alisema kuwa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo awali ulisainiwa na Katibu wa Nchi anayeshughulikia uhusiano ya Pande Mbili katika Wizara ya Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Mhe. Bi. Boglárka Illés na ilibaki upande wa Tanzania kutekeleza zoezi hilo.

Dkt. Mwamba alisema kuwa hatua ya kutiwa saini kwa upande wa Tanzania, inawezesha nchi kupata mkopo huo kupitia Benki ya Exim ya Hungary kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.

“Utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuboresha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi, sambamba na vipaumbele vya maendeleo ya Taifa vilivyoainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22–2025/26), Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 na Dira mpya ya Maendeleo ya Tanzania 2050”, alisema Dkt. Mwamba.

Alisema kuwa, pamoja na kuthamini mikopo nafuu, kuna umuhimu wa kupanua wigo wa ushirikiano ili kujumuisha pia misaada ya ruzuku katika maeneo kama vile ujenzi wa uwezo, elimu na sekta nyingine za kijamii, ili kuongeza manufaa jumuishi na endelevu kwa wananchi.

Alisisitiza dhamira thabiti ya Serikali ya kuendelea kuimarisha na kupanua ushirikiano wa pande mbili na Hungary chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kukuza ustawi wa wananchi wa nchi zote mbili.

Aidha Dkt. Mwamba alimpongeza Mhe. Balozi Nyirati kwa kuteuliwa kwake, akibainisha kuwa uteuzi huo unaakisi dhamira ya Serikali ya Hungary ya kuendeleza na kuimarisha mahusiano ya kihistoria na Tanzania pia alimhakikishia Balozi huyo ushirikiano kamili kutoka Serikali ya Tanzania katika kuendeleza uhusiano wa pande mbili.

Kwa upande wake Balozi Mteule wa Hungary nchini, Mhe. Katalin Nyirati, alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Hungary umedumu kwa zaidi ya miaka 60 kwa kuwa Tanzania ni mshirika wa kuaminika.

Aliihakikishia Tanzania kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo yenye manufaa kwa pande zote mbili ikiwa ni pamoja na ushirikiano katika sekta ya maji, elimu, kilimo, kisiasa na masuala ya teknolojia ambapo wako tayari kubadilishana ujuzi katika kuongeza ufanisi wa sekta hizo.

Alisema kuwa Dunia inapitia katika changamoto mbalimbali za kiuchumi hivyo ushirikiano wa dhati kati ya nchi hizo mbili utasaidia kuzihakikishia uimara wa kiuchumi na mambo mengine.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, aliishukuru Hungary kwa hatua iliyofikiwa ya utoaji wa mkopo wa mradi wa Maji Biharamulo, kwa kuwa wananchi wa eneo hilo wanasubiri kwa hamu utekelezaji wa mradi huo.


Alisema kuwa wananchi watafurahi kuona mkataba umesainiwa kwa kuwa unaleta matumaini mapya ya utekelezaji wa mradi huo wenye umuhimu mkubwa katika maendeleo.

No comments:

Post a Comment