WAZIRI HOMERA AWAHIMIZA MAWAKILI WA SERIKALI KUIMARISHA UWAJIBIKAJI NA KUPUNGUZA MIGOGORO YA KISHERIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 29, 2026

WAZIRI HOMERA AWAHIMIZA MAWAKILI WA SERIKALI KUIMARISHA UWAJIBIKAJI NA KUPUNGUZA MIGOGORO YA KISHERIA


Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Juma Homera,akizungumza katika mkutano wa mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi,akizungumza katika mkutano wa mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula,akizungumza katika mkutano wa mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) Bavoo Junus,akizungumza katika mkutano wa mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mawakili wa Serikali Tanzania, Ado Novemba,akizungumza katika mkutano wa mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Juma Homera (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Juma Homera (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Juma Homera (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.


Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA 


Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera amewataka mawakili wa Serikali nchini kuimarisha uwajibikaji na kufanya kazi kwa ufanisi ili kusaidia kupunguza migogoro isiyo ya lazima ambayo mara nyingi huchelewesha utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika kikao kazi cha mawakili wa Serikali, Dkt. Homera amesema kuwa wataalamu hao wanapaswa kutambua nafasi yao muhimu katika kutoa ushauri wa kisheria, hususan katika kipindi ambacho nchi inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati, hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa umakini na weledi wa hali ya juu.

Amesisitiza kuwa usimamizi thabiti wa mashauri ya kisheria ni nguzo muhimu katika kulinda rasilimali za umma na kuhakikisha haki inatendeka kwa kuzingatia misingi ya utawala bora na sheria, akionya kuwa uzembe mdogo unaweza kusababisha hasara kubwa kwa Serikali na wananchi kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, Waziri Homera amekipongeza Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) kwa kuendelea kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama wake, akibainisha kuwa hali hiyo ni msingi muhimu wa kuimarisha taaluma na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Amesisitiza umuhimu wa kuijenga taasisi hiyo kwa kuanzia ngazi ya chini hadi taifa kwa kuweka mifumo madhubuti ya kiutendaji, pamoja na kuwa na muundo thabiti unaojumuisha wataalamu wenye weledi na sekretarieti imara ili iweze kutoa huduma bora kwa wanachama wake na kuisaidia Serikali katika masuala ya kisheria.

Aidha, amependekeza kuanzishwa kwa mfuko maalumu wa maendeleo wa chama hicho utakaoimarisha ustawi wa wanachama na kuhakikisha uendelevu wa shughuli zake kwa muda mrefu.

Dkt. Homera amesisitiza kuwa Serikali ya Samia Suluhu Hassan inaendelea kuthamini mchango wa mawakili wa Serikali katika kulinda utawala wa sheria na kusimamia ipasavyo rasilimali za umma, akieleza kuwa mchango huo unasaidia kujenga imani ya wananchi kwa Serikali na kuhakikisha haki na usawa vinazingatiwa katika utoaji wa huduma za kisheria.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi amesema mkutano huo unapaswa kuwa chachu ya mabadiliko kwa kuweka msingi mpya wa sekta ya sheria na dira ya maendeleo hadi mwaka 2050.

Amesema ameshiriki mkutano huo si tu kama kiongozi bali pia kama mshiriki wa mageuzi ya sekta ya sheria, akiwataka wadau wote kushirikiana katika kujenga taasisi imara zitakazotoa huduma bora kwa wananchi katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.

Naye Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA), Bavoo Junus amesema chama hicho kinaendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili mawakili wa Serikali.

Awali, Mwenyekiti wa chama hicho, Ado Novemba amesema pamoja na mafanikio yaliyopatikana bado kuna changamoto za kiutendaji, ikiwemo tofauti za mishahara kwa watumishi kutoka taasisi na halmashauri mbalimbali, akiiomba Serikali kulifanyia kazi suala hilo ili kuleta usawa kazini.

Aidha, ameshauri kuimarishwa kwa programu za afya na mazoezi kwa watumishi ili kuboresha ustawi wao na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

No comments:

Post a Comment