
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Kushoto), akizungumza na Kiongozi wa Timu ya Wataalamu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) iliyofanya ziara nchini, Bw. Nicolas Blancher, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Timu ya Wataalamu wa Serikali ya Tanzania na Shirika hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam, ambapo Timu hizo zimefikia makubaliano ya ngazi ya wataalamu kuhusu ukamilishaji wa tathmini za mwisho za Mpango wa Extended Credit Facility-(ECF), na Resilience Sustainability Facility (RSF) hatua itakayoiwezesha Tanzania kupata ufadhili wa takribani dola za Marekani milioni 375.5, utakapo idhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya IMF.

Timu ya Wataalamu ya Serikali ya Tanzania ikiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Kulia) ikiwa katika kikao na Timu ya Wataalamu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ikiongozwa na Bw. Nicolas Blancher, kilichofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam, ambapo katika kikao hicho Timu hizo zimefikia makubaliano ya ngazi ya wataalamu kuhusu ukamilishaji wa tathmini za mwisho za Mpango wa Extended Credit Facility-(ECF), na Resilience Sustainability Facility (RSF) hatua itakayoiwezesha Tanzania kupata ufadhili wa takribani dola za Marekani milioni 375.5 utakapo idhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya IMF.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo wakati akiongoza Timu ya Wataalamu ya Serikali ya Tanzania, katika kikao na Timu ya Wataalamu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kilichofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam, ambapo katika kikao hicho Timu hizo zimefikia makubaliano ya ngazi ya wataalamu kuhusu ukamilishaji wa tathmini za mwisho za Mpango wa Extended Credit Facility-(ECF), na Resilience Sustainability Facility (RSF) hatua itakayoiwezesha Tanzania kupata ufadhili wa takribani dola za Marekani milioni 375.5, utakapo idhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya IMF.

Kiongozi wa Timu ya Wataalamu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) iliyofanya ziara nchini, Bw. Nicolas Blancher, akizungumza jambo wakati wa kikao na Timu ya Wataalamu ya Serikali ya Tanzania ikiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani), kilichofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam, ambapo katika kikao hicho timu hizo zimefikia makubaliano ya ngazi ya wataalamu kuhusu ukamilishaji wa tathmini za mwisho za Mpango wa Extended Credit Facility-(ECF), na Resilience Sustainability Facility (RSF) hatua itakayoiwezesha Tanzania kupata ufadhili wa takribani dola za Marekani milioni 375.5, utakapo idhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya IMF.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza katika kikao cha Timu ya Wataalamu ya Serikali ya Tanzania ikiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani) na Timu ya Watalaamu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) iliyofanya ziara nchini, kilichofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam, ambapo katika kikao hicho Timu hizo zimefikia makubaliano ya ngazi ya wataalamu kuhusu ukamilishaji wa tathmini za mwisho za Mpango wa Extended Credit Facility-(ECF), na Resilience Sustainability Facility (RSF) hatua itakayoiwezesha Tanzania kupata ufadhili wa takribani dola za Marekani milioni 375.5, baada ya kuidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya IMF.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Sebastian Acevedo, wakiteta jambo mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Timu ya Wataalamu wa Serikali ya Tanzania na IMF, kilichofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam, ambapo timu hizo zimefikia makubaliano ya ngazi ya wataalamu kuhusu ukamilishaji wa tathmini za mwisho za Mpango wa Extended Credit Facility-(ECF), na Resilience Sustainability Facility (RSF) hatua itakayoiwezesha Tanzania kupata ufadhili wa takribani dola za Marekani milioni 375.5 baada ya kuidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya IMF.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)
Na Joseph Mahumi, WF, Dar es Salaam
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Serikali ya Tanzania zimefikia makubaliano ya ngazi ya wataalamu kuhusu ukamilishaji wa tathmini za mwisho za Mpango wa Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii na Resilience Sustainability Facility (RSF) ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, hatua itakayoiwezesha Tanzania kupata ufadhili wa takribani dola za Marekani milioni 375.5 baada ya kuidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya IMF.
Fedha hizo kiasi cha dola za Marekani milioni 375.5 kitaifanya Tanzania inufaike na mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.052 za kusaidia miradi ya kiuchumi na kiasi kingine cha dola za Marekani milioni 563.8 za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi tangu utekelezaji wa program hizo uanze.
Hayo yamebainishwa na IMF kupitia Kiongozi wa Timu ya Wataalamu ya Shirika hilo iliyofanya ziara nchini, Bw. Nicolas Blancher, baada ya kikao cha kuhitimisha ziara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam, huku Timu ya Tanzania ikiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb).
Akitoa taarifa hiyo Kiongozi wa Timu ya Wataalamu ya Shirika hilo, Bw. Nicolas Blancher, alisema kuwa IMF imeridhishwa na utekelezaji wa programu hizo mbili huku ikibainisha kuwa malengo makuu ya kiuchumi yamefikiwa kwa kiwango kikubwa.
Bw. Blancher alisema kuwa malengo mapana ya programu hizo yamefikiwa, ukuaji wa uchumi umeendelea kuwa imara, mfumuko wa bei umeendelea kuwa thabiti na ndani ya kiwango kinacholengwa na Benki Kuu ya Tanzania, kiwango cha akiba ya fedha za kigeni kimeendelea kuwa katika kiwango cha kuridhisha, huku matumizi ya Serikali katika sekta za elimu na afya yakiongezeka sambamba na hatua za kuimarisha ustahimilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.
“Serikali imeimarisha uthabiti wa uchumi jumla, imeongeza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na hatari nyingine za kiuchumi” alisema Bw. Blancher
Aliongeza kuwa uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.9 mwaka 2026 huku mfumuko wa bei ukitarajiwa kubaki ndani ya lengo la Benki Kuu ya Tanzania la asilimia 3 hadi 5, na Taasisi hiyo imepongeza namna Serikali ilivyoweza kukabiliana na athari za changamoto za kiuchumi duniani ikiwemo vita vya Mashariki ya Kati kupitia sera madhubuti za kifedha na fedha.
“Utekelezaji thabiti wa bajeti, ukusanyaji mzuri wa mapato ya kodi, pamoja na kuendelea kulipa marejesho ya kodi na madeni ya ndani kwa wakati, ni hatua muhimu zitakazosaidia kuendeleza ukuaji wa sekta binafsi na kulinda matumizi ya kijamii katika afya, elimu na ulinzi wa jamii” alisema Bw. Blancher.
IMF imesema kuwa katika kipindi cha kati na mrefu, Tanzania ina nafasi nzuri ya kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ikiwa itaendelea kutekeleza mageuzi yatakayokuza mtaji rasilimali watu, kuboresha mazingira ya biashara, kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi na kuimarisha usimamizi wa fedha za umma.
“Kwa kuendeleza mafanikio yaliyopatikana chini ya programu zinazoungwa mkono na ECF na RSF, ukuaji na maendeleo ya uchumi wa Tanzania yatategemea kuharakishwa kwa mageuzi ili kufikia malengo makubwa yaliyowekwa katika Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050, hususan katika maeneo ya maendeleo ya rasilimali watu na sekta binafsi” alisema Bw. Blancher
IMF ilihitimisha kwa kusema kuwa, Vipaumbele muhimu ni pamoja na kuongeza zaidi mapato ya ndani ili kuunda nafasi ya kifedha kwa matumizi ya kijamii yenye kipaumbele huku ikiendelea kudumisha uwekezaji katika miundombinu; kuimarisha usimamizi wa fedha za umma na uwekezaji; kuendeleza uhuru wa Benki Kuu; pamoja na kuboresha mazingira ya biashara.
Mageuzi endelevu ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi pia yatasaidia kuongeza ustahimilivu na uendelevu wa uchumi, ikiwemo kwa kupanua mifumo ya hifadhi ya jamii na kusaidia uwekezaji katika nishati jadidifu.
Akizungumza kuhusu hatua hiyo ya mafanikio makubwa ya utekelezaji wa program hizo, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), alisema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza program hizo kwa umakini mkubwa ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Aliihakikishia IMF kuwa Tanzania itaendelea kuwa makini katika matumizi ya Fedha hizo ili malengo yaliyowekwa ya kuwa na uchumi imara, thabiti na jumuishi yanafikiwa na kuleta tija kwa uchumi wa Taifa na maendeleo ya watu.

No comments:
Post a Comment