JIJI LA DODOMA LATOA VIWANJA 1,900 KWA WAFANYAKAZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 1, 2026

JIJI LA DODOMA LATOA VIWANJA 1,900 KWA WAFANYAKAZI



Na. Mwandishi wetu, DODOMA


HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeibuka kivingine katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa kuachia viwanja zaidi ya 1,900 vya matumizi mbalimbali kwa ajili ya wafanyakazi na wananchi kwa ujumla ili waweze kufurahia fursa ya kumiliki kiwanja katika makao makuu ya nchi.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dennis Gondwe alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu nafasi ya Halmashgauri ya Jiji la Dodoma katika kujali makazi ya wafanyakazi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika ngazi ya mkoa katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

“Nitumie nafasi hii kuwashauri na kuwashawishi wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma na wengine wote kuhakikisha wananunua viwanja katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Hii itaweka alama kwa utumishi wao katika halmshauri, lakini kwa wale walio nje ya halmshauri itaweka alama kwa kumiliki kiwanja kihalali katika makao makuu ya nchi. Wote tu mashahidi kwamba kila mtanzania anatamani awe sehemu ya makao makuu, wakati uliokubalika ni sasa.

 Ardhi haiongezeki, ila inapanda thamani kila uchwao. Natamani kupitia Meimosi hii ya Mwaka 2026, kila mfanyakazi aweke alama kwa kununua kiwanja katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, makao makuu ya nchi. Na alama hii ili iwe kumbukumbu kwa wengi, mshawishi hata mwenzako ambae siyo mfanyakazi kununua kiwanja. 

Pamoja na kuweka alama, pia ni kuunga mkono maono ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule kupitia kaulimbi ya Dodoma ni fahari ya watanzania” alisema Gondwe.

Akiongelea mchakato wa kununua viwanja hivyo, alisema kuwa serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi imerahisisha mchakato huo. “Sasa hakuna sababu ya kupanga foleni kwa ajili ya kununua kiwanja, hakuna sababu ya kusafiri kwa ajili ya kuja Dodoma kununua kiwanja.

Ingia www.tausi.tamisemi.go.tz jisajili na tafuta Halmashauri ya Jiji la Dodoma nunua kiwanja. Hata mchakato wa upatikanaji wa hati umerahisishwa, utaingia e-ardhi na kufanya maombi ya hati mahali popote ulipo. Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeachia viwanja zaidi ya 1,900 vya makazi, biashara, makazi na biashara, taasisi na viwanda katika maeneo ya Nala, Mahomanyika na Kikombo kwa ajili ya watanzania kuvinunua” alisema Gondwe.

Kwa upande wake Mfanyakazi hodari zaidi ya mara moja kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Theresia Nkwanga alisema kuwa ni heshima kwa mfanyakazi kumiliki kiwanja katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Ukuaji wa makao makuu ya nchi Dodoma ni wa kasi kubwa. Hivyo, fursa zilizopo katika ardhi hazina mjadala mpana. Ni kumbukumbu nzuri kwa mfanyakazi na kizazi chake kuwa historia na sehemu ya mafanikio ya Dodoma kwa kumiliki kiwanja halili sasa. Hakika Jiji la Dodoma limekuja kivingine” alisema Nkwanga.


Maadhimisho ya Meimosi mwaka 2026 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Kazi zenye Staha ni Nguzo imara kwa Maendeleo Endelevu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050”.

No comments:

Post a Comment