MIGODI YA BARRICK YASHINDA TUZO 11 ZA OSHA 2026 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, May 3, 2026

MIGODI YA BARRICK YASHINDA TUZO 11 ZA OSHA 2026


Naibu Katibu Mkuu-Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi,Ajira na Mahusiano, Zuhura Yunus (kushoto) akimkabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza katika kipengele cha usambazaji maji na udhibiti wa Maji taka na shughuli za urekebishaji, Afisa Rasilimali Mwandamizi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Renatus Malawa wakati wa hafla ya tuzo za OSHA 2026 zilizofanyika mjini Njombe. Migodi ya Barrick nchini ilishinda tuzo 11.

Naibu Katibu Mkuu-Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Zuhura Yunus (kushoto) akimkabidhi tuzo ua ushindi ,Mrakibu Mwandamizi wa Usalama kutoka Mgodi wa Barrick North Mara, Meshack Issack wakati wa hafla ya tuzo za OSHA 2026 zilizofanyika mjini Njombe. Migodi ya Barrick nchini ilishinda tuzo 11.

Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakisherekea ushindi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mjini Njombe.

Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakisherekea ushindi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mjini Njombe.

***

Migodi ya Bulyanhulu na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga imeendelea kudhihirisha kuwa ni mahiri katika kutekeleza kwa vitendo kanuni za Afya na Usalama Mahali pa Kazi ambapo imenyakua tuzo 11 katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) kwa mwaka 2026 iliyofanyika mjini Njombe.

Mgodi Barrick Bulyanhulu uliopo latika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga umeshinda tuzo 7 na Mgodi wa Barrick North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara umeshinda tuzo 4.

Tuzo ambazo mgodi wa Bulyanhulu umeshinda ziko katika vipengele vya Mwonyeshaji bora (Best OHS Exhibitor), Ubunifu (Innovation), shughuli za uchimbaji madini (Mining Activities), usambazaji maji na udhibiti maji taka na shughuli za urekebishaji (Water Supply, Sewerage Management and Remediation Activities), shughuli za upasuaji miamba (Quarrying Activities), utengenezaji mashine na mitambo na bidhaa za chuma (Manufacturer of Machinery and Equipment and Fabricated Metal Products) na utengenezaji wa wa awali wa vito na metali nyingine zisizo na chuma (Manufacturing of Basic Precious and other Non-ferrous Metals).

Barrick North Mara imenyakua tuzo za usambazaji maji na udhibiti wa Maji taka na shughuli za urekebishaji (Water Supply, Sewerage Waste Management and Remediation Activities), maudhui ya maonesho (OHS Exhibitor Theme, Ubunifu (innovation) na shughuli za upasuaji miamba (Quarrying Activities).

Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mh.Deus Sangu, ambaye alisisitiza umuhimu wa waajiri na wafanyakazi kuzingati sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na serikali kupitia Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) ili kumlinda mfanyakazi na uwekezaji na biashara kwa ujumla vilevile aliwapongeza washiriki wote na wadhamini wa maonesho ya mwaka huu.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda, alitumia nafasi hiyo kuwashukuru washiriki wote, waajiri na wafanyakazi kwa kuendelea kuzingatia kanuni na sheria za afya na usalama mahali pa kazi kama injini ya kuongeza uzalishaji kwenye maeneo yao ya kazi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchini wa taifa kwa ujumla.

Ushindi wa mwaka huu wa tuzo 11 ni mwendelezo wa ushindi katika maonesho ya OSHA yaliyofanyika katika miaka ya karibuni, ambapo mwaka jana pia kampuni ya Barrick ilishinda tuzo 10 na mwaka juzi ilishinda tuzo tano, ikiwemo tuzo ya mshindi wa jumla kupitia mgodi wa Bulyanhulu.

Suala la Afya na Usalama ni DNA ya kampuni ya Barrick ambapo inatekeleza programu ya usalama ya ‘Journey to Zero’ inayolenga kufanikisha kutokomeza matukio ya ajali kazini na nje ya kazi kwa wafanyakazi wake.

Programu hii pia imevuka maeneo ya migodi na sasa inawafikia wananchi kwenye jamii zinazoishi jirani na migodi vilevile wataalamu wa usalama kutoka Barrick, katika maonesho ya mwaka huu wameendesha mafunzo ya usalama na udhibiti wa majanga ya moto kwa wanachi wa mkoa wa Njombe.

Mbali na kuwekeza katika usalama, Barrick imeendelea kuchangia pato la Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali, gawio na kufanikisha kutekeleza miradi mikubwa ya kijamii kupitia fedha za CSR zinazotolewa na migodi yake, hususan katika sekta za afya, elimu ,maji safi ya kunywa na miundombinu ya barabara ambayo imebadilisha maisha ya wananchi kuwa bora zaidi.

Pia, kampuni ya Barrick imekuwa kinara wa kutekeleza sera ya maudhui ya ndani (Local content) ambayo inaendelea kuwanufaisha wazawa kwa kufanya kazi na migodi yake.

Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakisherekea ushindi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mjini Njombe


Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakisherekea ushindi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mjini Njombe

Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakisherekea ushindi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mjini Njombe


Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakisherekea ushindi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mjini Njombe







No comments:

Post a Comment