UTT AMIS YASHIRIKI MEI MOSI, YAHAMASISHA WANANCHI KUWEKEZA MIFUKO YA PAMOJA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 1, 2026

UTT AMIS YASHIRIKI MEI MOSI, YAHAMASISHA WANANCHI KUWEKEZA MIFUKO YA PAMOJA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mfuko wa uwekezaji nchini, UTT AMIS, umehimiza wananchi kutumia fursa ya kuwekeza katika mifuko mbalimbali ya uwekezaji wa pamoja ili kuongeza thamani ya fedha zao na kupata faida shindani.

Akizungumza leo, Mei 1, 2026, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika viunga vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Afisa wa UTT AMIS, Bw. Brayan Kiwele, alisema uwekezaji hauhitaji kuwa na mtaji mkubwa kama ambavyo wengi hudhani.

Alifafanua kuwa wananchi wa kipato cha chini, cha kati na hata cha juu wanaweza kuwekeza fedha zao kupitia mifuko hiyo na kuona ongezeko la thamani kwa muda.

“Watanzania wengi wakisikia uwekezaji, jambo la kwanza kufikiria ni kuwa unahitaji fedha nyingi. Lakini hata mwenye mtaji mdogo anaweza kuanza na kunufaika,” alisema.

Aidha, alieleza kuwa mchakato wa kujiunga na mifuko ya uwekezaji ya UTT AMIS ni rahisi, kwani unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yao au kwa kutumia programu ya simu inayopatikana katika Google Play Store.

UTT AMIS imeendelea kusisitiza umuhimu wa uwekezaji kwa wananchi kama njia ya kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kukuza uchumi binafsi na wa taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment