WADAU JIJINI DAR ES SALAAM WASHIRIKI MAPITIO YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA KUENDANA NA DIRA 2050. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 6, 2026

WADAU JIJINI DAR ES SALAAM WASHIRIKI MAPITIO YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA KUENDANA NA DIRA 2050.


Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bi Emma Komba, akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha kufanya mapitio ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Sheria Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Paul Kadoshi, akifafanua jambo kuhusiana na mchakato wa zabuni, katika kikao kazi cha kufanya mapitio ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina, jijini Dar es Salaam.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bi Emma Komba, na Mkurugenzi wa Sheria Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Paul Kadoshi, wakifuatilia maoni ya wadau katika kikao kazi cha kufanya mapitio ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi Benki ya NBC, Bi. Sesaria Kusimbi, akitoa maoni katika kikao kazi cha kufanya mapitio ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau wakifuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa katika kikao kazi cha kufanya mapitio ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina, jijini Dar es Salaam.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bi. Emma Komba, akiwa katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki katika kikao kazi cha kutoa maoni na kufanya mapitio ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina, jijini Dar es Salaam.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam.)


Na. Saidina Msangi, WF, Dar es Salaam.


Wizara ya Fedha imeendelea na mchakato wa kupitia upya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kupitia kikao kazi kilichowakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi.

Wizara imeendelea na mchakato huo ikiwa ni kikao kazi cha pili kufanyika ambapo wadau mbalimbali walipata fursa ya kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha Sheria hiyo, katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Hazina, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bi Emma Komba, alisema mapitio hayo yanalenga kujenga mfumo wa kisasa unaojumuisha hatua zote za mnyororo wa ugavi, kuanzia upangaji wa mahitaji, ununuzi, upokeaji na ugomboaji, uhifadhi na utunzaji, usambazaji, hadi uondoshaji wa mali.

Alisisitiza kuwa mapitio hayo ni hatua ya kimkakati ya kuhakikisha kuwa masuala yote yanayohusu mnyororo mzima wa ugavi yanajumuishwa kikamilifu katika Sheria mpya, na kwamba mageuzi hayo yatakuwa chachu ya kuchochea maendeleo ya Taifa.

Bi. Komba aliwahimiza wadau wote kushiriki kikamilifu kutoa maoni na kukisisitiza kuwa ushiriki wao ndio utakaohakikisha Sheria mpya inakuwa bora, jumuishi na yenye tija kwa maendeleo ya Taifa kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo 2050.

Kikao hicho, kilichoratibiwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, kiliwakutanisha pamoja wadau mbalimbali kutoka Sekta ya umma na binafsi.

Kwa upande wa sekta ya umma, taasisi zilizoshiriki ni pamoja na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), TANROAD, SUMAJKT pamoja na Benki ya Maendeleo ya TIB.

Kwa upande wa sekta binafsi, walishiriki walikuwa Benki ya NBC, Soft tech consultancy, Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Cross World Travel Agent Limited, Masasi Construction, pamoja na Perfect Infotech International, ambao walipata fursa ya kuwasilisha maoni yao kuhusu namna ya kuboresha mazingira ya biashara na ushiriki wao hasa kuwawezesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kushiriki katika shughuli za ununuzi wa umma na ugavi.

No comments:

Post a Comment