WAKENYA WAASWA KUACHA KUWADHARAU WATANZANIA NA WATANZANIA KUACHA KUWAOGOPA WAKENYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 6, 2026

WAKENYA WAASWA KUACHA KUWADHARAU WATANZANIA NA WATANZANIA KUACHA KUWAOGOPA WAKENYA

Mfanyabiashara nguli na Mwenyekiti wa Taifa Group , Rostam Azizi akizungumza kwenye mkutano wa Biashara kati ya Kenya na Tanzania uliyofanyika jijini Dar es Salaam.

*

Mkutano wa siku moja wa biashara kati ya Tanzania na Kenya uliofanyika Jumatatu wiki hii jijini Dar es Salaam ulikuwa na mambo mengi na mikakati ya kuimarisha umoja baina ya wananchi wa nchi hizi mbili.

Moja ya hotuba ya kihistoria ya kuwatia moyo wananchi wa nchi hizi mbili katika safari ya kuelekea kwenye ushirikiano wa kweli kibiashara unaoashiria kuleta mafanikio ilitolewa  na Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Taifa Group,  Rostam Azizi mbele ya Ma Rais wa nchi hizi, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dk.William Ruto.

Alisema wananchi wa wakenya na wa Tanzania wanapaswa kushirikiana na hakuna ambaye yupo juu ya mwenzake katika nyanja  za biashara, mitaji na uchumi.

 “Ni muhimu Wakenya kukubali kwamba Watanzania wamekua na tupo kimo kimoja hivyo tunapaswa kuchukua hatua na historia mpya katika muktadha wa kujenga mfungamano wa kweli wa kiuchumi na kubadilisha mustakabali wa nchini hizi mbili”, alisisitiza.

Rostam alisema muktadha huu mpya wa dunia, Tanzania na Kenya zina nafasi ya kipekee ya kimkakati, alisisitiza na kuongeza kuwa Wakenya waache kufurahia, kusherekea au kushabikia watanzania wanapopata majanga au taharuki mbalimbali na Watanzania wasiwaone Wakenya ni tishio kwenye biashara na ajira.

Alisema tunapakana na masoko mengi ya kikanda, tuna bandari muhimu katika Bahari ya Hindi, na tupo kwenye njia kuu za biashara za dunia. Kwa lugha rahisi, sisi ndiyo lango la biashara la Bara letu la Afrika.

Aliongeza kwamba ni nafasi ya kipekee kwa watanzania na wakenya kufanya kazi kwa kushirikiana na si kwa kutengana kwa sababu nchini hizi zinahitajiana.

Hotuba ya kusisitiza ushirikiano baina ya mataifa ya Tanzania sio mara ya kwanza kutolewa na mfanyabiashara huyu,hivi karibuni akiongea na waandishi wa habari jijini Nairobi alisema Tanzania na Kenya sio maadui na washindani bali zinapaswa kushirikiana na kusaidiana.

Aliongeza kwamba hakuna kaka mkubwa katika ushirikiano huo wa kibiashara na mitaji kati kenya na Tanzania bali wanapaswa kushirikiana kwa pamoja ili kukuza mitaji , kuongeza ufanisi wa biashara , mitaji na uwekezaji mkubwa kwenye miradi yenye maslahi mapana kwa nchini hizo mbili.

Alisisitiza kwenye mkutano huo  kwamba hakuna mkubwa dhidi ya mwenzake , watanzania na wakenya wote wapo sawa (we are equals).

No comments:

Post a Comment