RATIBA ROBO FAINALI KOMBE LA CHALLENGE 2015
Novemba 30, 2015
Uganda Vs Malawi (Saa 8:00 mchana)
Tanzania Bara Vs Ethiopia (Saa 10:00 jioni)
Desemba 1, 2015
Sudan Kusini Vs Sudan (Saa 8:00 mchana)
Rwanda Vs Kenya (Saa 10:00 jioni)
Uganda Vs Malawi (Saa 8:00 mchana)
Tanzania Bara Vs Ethiopia (Saa 10:00 jioni)
Desemba 1, 2015
Sudan Kusini Vs Sudan (Saa 8:00 mchana)
Rwanda Vs Kenya (Saa 10:00 jioni)
![]() |
John Bocco (kulia) amesema watapambana kiume leo waitoe Ethiopia |
NAHODHA
wa Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Stars’ amesema kwamba watapigana ‘kufa
na kupona’ kuhakikisha wanawatoa Ethiopia leo katika Ratiba Robo Fainali
Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.
“Ni
mchezo mgumu, kwa sababu wao wanacheza nyumbani na tumekwishaona jinsi
wanavyopewa sapoti na mashabiki wa kwao. Kwa kweli utakuwa mtihani
mgumu, lakini sisi tumejipanga,”amesema Bocco.
Robo
Fainali za CECAFA Challenge zinaanza leo katika Uwanja wa Taifa wa
Addis Ababa, Ethiopia, mechi ya kwanza ikizikutanisha Uganda na Malawi
na baadaye Tanzania Bara na Sudan. Hatua hii itahitimishwa kesho kwa
michezo mingine miwili ya Robo Fainali, wa kwanza ukizikutanisha Sudan
Kusini na Sudan na wa pili ukiwakutanisha Rwanda na Kenya.
Bocco
amesema wanaomba Mungu awajaalie washinde mchezo wa leo na kwenda Nusu
Fainali, ili kurejesha imani ya Watanzania kwa timu zao za taifa.
“Tunajua
tuna deni kubwa kwa Watanzania, kwa kweli tutajitahidi sana tuweze
kufanya vizuri ili wananchi warejeshe imani na timu yao,”amesema Bocco.
Tanzania Bara na Ethiopia zote zimetoka Kundi A na mechi baina yao zilitoka sare ya 1-1, hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mkali zaidi.
Tanzania Bara na Ethiopia zote zimetoka Kundi A na mechi baina yao zilitoka sare ya 1-1, hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mkali zaidi.
Bara
imepita kama mshindi wa kwanza wa Kundi A, wakati Ethiopia imepenya
kwenye tundu la sindano kama mshindi wa tatu bora namba mbili, nyuma ya
Sudan.
Bara, Rwanda kutoka Kundi A, Uganda, Kenya kutoka Kundi B na Sudan Kusini na Malawi kutoka Kundi C hizo ndizo zimefuzu kwa kushika nafasi mbili za juu kwenye makundi yao.
Bara, Rwanda kutoka Kundi A, Uganda, Kenya kutoka Kundi B na Sudan Kusini na Malawi kutoka Kundi C hizo ndizo zimefuzu kwa kushika nafasi mbili za juu kwenye makundi yao.
No comments:
Post a Comment