NACTVET ,KUFANYA UTAFITI WA PROGRAMU PAMOJA NA KUANDAA MITAALA ITAKAYOMSAIDIA MWANAFUNZI KUKIDHI MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, April 1, 2022

NACTVET ,KUFANYA UTAFITI WA PROGRAMU PAMOJA NA KUANDAA MITAALA ITAKAYOMSAIDIA MWANAFUNZI KUKIDHI MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA.

Mkuu wa Kanda ya kati wa NACTVET, Bw. Ramadhan  Semainda wakati wa Mafunzo Endelevu ya Wataalam(CPD) ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi April 1,2022 hapa jijini Dodoma kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) ya Kuwajengea Uwezo Wataalam wa kushiriki kwenye Miradi mikubwa.

Isome hapa maana ya NACTVET

Na Okuly Julius Dodoma

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) ina majukukumu makubwa Ikiwemo kuandaa Mitaala na kufanya utafiti juu ya programu zilizopo katika soko la Ajira.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kanda ya kati wa NACTVET, Bw. Ramadhan  Semainda wakati wa Mafunzo Endelevu ya Wataalam(CPD) ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi April 1,2022 hapa jijini Dodoma kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) ya Kuwajengea Uwezo Wataalam wa kushiriki kwenye Miradi mikubwa.

Pia ameongeza kuwa NACTVET mbali na kuwa na jukumu la kuandaa na kuhakikisha vyuo vyote ambavyo sio vyuo vikuu vinasajiliwa pamoja na kutoa elimu bora wana jukumu kubwa pia la kuvishauri vyuo hivyo katika baadhi ya programu ili wakati wanafunzi wanasoma wajue kabisa uhalisia wa Soko la Ajira.

Hivyo Baraza limeanzisha mfumo wa CBET ambao kazi yake kubwa ni kuhakikishe inamuandaa mwanfunzi kuwa na ujuzi na umahiri ili anapomaliza mafunzo yake aweze kujiajiri au kuajirika.

Pamoja na hayo amefafanu kuhusu Elimu ya Ufundi kuwa ni ule ujuzi na umahiri anaoupata mtu baada ya kusoma hivyo kila mmoja kulingana na kazi yake ana ujuzi aliyoupata na hapo ndipo umuhimu wa vyuo vya ufundi unapopatikana.

" Kila mmoja kwa fani yake anatumia ufundi hata Madaktari,Wahasibu na watu wenye fani tofauti tofauti hivyo ifike mahali watu wazingatie elimu hii kwa sababu inatumika katika nyanja mbalimbali za ajira,"Amesema Ramadhani Semainda.

Ikumbukwe, NACTVET imekuja baada ya serikali kufanya mabadiliko madogo kwenye Sheria ya NACTE Septemba mwaka 2021 kwa kuongeza jukumu la urekebu kwenye vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi ili kuwatengeneza vijana  wa Kitanzania wawe na ujuzi na umahiri unaokidhi matakwa ya  soko la ajira katika programu wanazojifunza.

TAZAMA VIDEO HAPO CHINI MKUU WA UKANDA WA KATI NACTVET AKIFAFANUA JUU YA MFUMO WA CBET

No comments:

Post a Comment