Na Okuly Julius-Dodoma
Katika kuhakikisha kuwa kongamano la maboresho ya Sera ya elimu ya mwaka 2014 na mabadiliko ya mitaala ya elimu hapa nchini linafanikiwa kwa viwango vikubwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesogeza mbele kongamano hilo lililokuwa lifanyike tarehe 13 hadi 15 mwezi huu.
Lengo la kusogeza mbele kongamano hilo ni kutoa wigo mpana kwa wadau mbalimbali kuendelea kujisajili kwa ajili ya kushiriki kutokana na maoni ya wadau.
Kwa mujibu wa Waziri Prof.Adolf Mkenda ambaye siku zote amekuwa akizungumzia kuhusu maboresho ya Elimu hapa nchini amesema ili elimu yetu iendelee kuwa bora ni lazima Sera,Sheria na Mitaala ibadilike ili kukidhi mahitaji halisi ya kitaifa na kimataifa ya sasa na baadae.
Lakini ameongeza kuwa ili kufikia mabadiliko hayo ni vema kuhakikisha wadau wote wanapata fursa ya kushiriki kutoa maoni kabla na baadae wataalamu watafanya uchambuzi wa kitaalamu.
Hivyo ukiwa kama mdau wa elimu usichelewe kuendelea kutoa maoni na kujisajili ili kushiriki katika majadiliano hayo.
ENDELEA KUTOA MAONI KUPITIA
maoniyawadau@tie.go.tz au
info@moe.go.tz
au tupigie kwa Namba
0735041169
TUTAKUSIKILIZA
No comments:
Post a Comment