
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi,akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa TALGWU Taifa Bw.Tumaini Nyamhokya,akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Ndg. Rashid Mtima,akitoa taarifa ya Kikao cha Baraza Kuu TALGWU Taifa kilichofanyika leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.

BAADHI ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi (hayupo pichani), wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.
Na Okuly Julius-Dodoma
Naibu Waziri Ofisini ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Patrobas Katambi amewataka waajiri kuhakikisha wanafuata matakwa ya sheria za kazi za nchi na kudumisha mahusiano mema kazini kwa manufaa yao wenyewe na wafanyakazi wao.
Katambi ameyasema hayo Leo Januari 15,2023 Jijini Dodoma wakati akifungua kikao Cha Baraza Kuu la chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) chenye lengo la kupitia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Chama hicho, taarifa ya fedha kwa mwaka 2023 pamoja na kufanya kazi ya kupitia na kuidhinisha makisio ya mapato na matumizi ya Chama hicho kwa mwaka wa fedha 2024.
Ambapo Katambi ,amesema Serikali itaendelea kulinda na kuendeleza haki za wafanyakazi nchini huku ikitambua, kuheshimu na kuuenzi mchango wa Watumishi wa Umma ambao ni Wanachama TALGWU.
"Waajiri kuhakikisha wanafuata matakwa ya sheria za kazi za nchi na kudumisha mahusiano mema kazini kwa manufaa yenu wenyewe na wafanyakazi wenu na Utashi wa Serikali katika kutekeleza wajibu wake wa kulinda haki za wafanyakazi nchini umejidhihirisha wazi kupitia hatua za kisheria na za kiuchumi ambazo imekuwa inatekeleza,"
Na kuongeza kuwa"Tunatambua kuwa wengi wenu mnafanya kazi katika mazingira magumu lakini Serikali haitachoka kuzifanyia kazi kero na changamoto zenu na kutafuta njia mbalimbali za kuzipatia ufumbuzi sambamba na kuendelea kuboresha mazingira ya kazi,"amesema Katambi
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TALGWU Rashid Mtima amesema kati ya changamoto zinazowakabili wanachama wao hasa wa Kada ya Afya( madaktari,wauguzi,wafamasia,wataalamu wa Maabara, wataalamu wa Mionzi na Wafiziotherapia) ni kulipa leseni za kutolea hudumu huku wakiwa wanatoa huduma kwa jamii hivyo kuomba waajiri kuwalipia gharama hizo za leseni na Leseni ya kutoa huduma isiwe sehemu ya kigezo cha watumishi wa kada ya Afya kupandishwa madaraja.
Pia amesema kuna changamoto katika miundo ya utumishi hasa katika kupandishwa vyeo na kubadilishwa muundo (promotion and Recategorization) ambapo changamoto katika miundo ya kiutumishi kwa kada za Watumishi ambao sio Walimu , wanapotaka kubadili muundo pindi wanapotoka masomoni kujiendeleza muundo unamlazimu kupelekwa katika cheo cha chini cha kuanzia bila kuzingatia uzoefu katika utumishi wa Umma.
Akijibu Changamoto hizo Naibu Waziri Katambi amewahakikishia TALGWU kuwa Serikali imesikia, imeelewa na ipo tayari kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha wafanyakazi wanatekeleza majukumu yao kwa amani huku changamoto walizonazo zikiwa zinapatiwa ufumbuzi na serikali chini ya uongozi madhubuti wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Pia amewataka wanachama wote wa TALGWU kutambua kuwa ulinzi wa haki za wafanyakazi huanzia kwa wao wenyewe kwa kuzingatia dhana ya haki na wajibu,hivyo Chama hicho kinapaswa kuwakumbusha wafanyakazi kujiepusha na vitendo vinavyoenda kinyume na misingi na maadili ya Utumishi wa Umma.
"Wafanyakazi kama hawatajiepusha na matendo hayo maovu basi watafanya kazi ya kutetea na kulinda haki zao kuwa ngumu kwao na wadau wengine kama sisi. Lazima wakati wote tukumbuke kuwa kudai haki kunaenda sambamba na kutimiza wajibu,"amesisitiza Katambi
No comments:
Post a Comment