Dar Es Salaam, Julai 19, 2024.
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza rasmi matokeo ya mitihani ya 28 ya PSPTB iliyofanyika kuanzia 13 Mei hadi 17 Mei, 2024 katika vituo sita vya mitihani Tanzania bara na Visiwani.
Akitangaza matokeo hayo Mkururugenzi Mtendaji - PSPTB , Godfred Mbanyi
amesema jumla ya watahiniwa wapatao 1,280 walisajiliwa ili kufanya mitihani huo ambapo watahiniwa 1,197 (93.5%) walifanya mitihani hiyo ikiwa ni ongezeko la watahiniwa ukilinganisha na msimu uliopita ulikuwa na watahinwa 977.
Taarifa ya matokeo ya mitihani ya 28 ya PSPTB ni kama ifuatavyo:
Kati ya watahiniwa 1,280 Jumla ya watahiniwa 551 sawa na 46.0% wamefaulu mitihani yao, watahiniwa 632 sawa na 52.8% watarudia baadhi ya masomo kuanzia somo moja mpaka masomo matatu kutegemeana na masomo idadi ya masomo aliyofeli, na watahiniwa 14 sawa na 1.2% wamefeli masomo yote waliyofanya katika ngazi zao.
Katika masomo 39 waliyopimwa watahiniwa,masomo 24 yalifanywa vizuri, 07 yalifanywa kwa wastani na masomo 08 yalikuwa chini ya WASTANI.
Kwa ujumla watahiniwa wa kike walifanya vizuri ukilinganisha na watahiniwa wa kiume. Katika ufaulu wa jumla watahiniwa wawili wakike wakiibuka watahiniwa bora katika ngazi za mitihani za Graduate Professional I, na CPSP.
Mikakati ya PSPTB kwa siku za mbele
MOJA : Kuendelea kuimarisha na kusimamia ubora wa mafunzo yanayotolewa na vituo vya kuwaandaa watahiniwa review centers
Kuendelea kuimarisha mahusiano ya kitaaluma na Taasisi za elimu ya Juu na Kati ili kuongeza ubora na ufaulu katrika mitihani ya PSPTB,
MBILI : Kuendelea kuhimiza na kusimamia uanzishwaji na uendeshaji wa mafunzo kwa kutumia fursa ya nyezo za mitandao zilizopo.
TATU : Kuendelea kufanya ziara za kimafunzo vyuoni na katika vito vya mafunzo vilivyosajiliwa na PSPTB ili kuhamasisha usomaji wenye tija kwa ajili ya utendaji mzuri katika mitihani ya PSPTB,
NNE : Kuendelea kutembelea vyuo mbalimbali vinavyofundisha taaluma ya Ununuzi, Ugavi, Usafirishaji , kushiriki maonesho mbalimbali yakiwemo ya kitaaluma na kutoa aelimu ya umuhimu wa kufanya mitihani ya PSPTB.

No comments:
Post a Comment