Wizara ya Maji inashirikiana na wadau mbalimbali ili kuwa na mfumo madhubiti wa kusimamia miradi ya maji hasa kwa maeneo ya vijijini kwa kushirikiana na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)
Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Alex Tarimo amesema hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji jijini Dodoma wakati wa kikao kazi na Taasisi ya Kidini chini ya kanisa la Anglikana kilichojadili mfumo wa utekelezaji wa miradi ya maji inayotekelezwa na Taasisi hiyo katika mikoa ya Lindi, Ruvuma na Mtwara
kwa ushirikiano na Serikali.
Lengo la kikao hicho likiwa kuendelea kushirikisha Sekta Binafsi katika kufikisha huduma endelevu ya maji bila kikwazo kwa wananchi.
Kiongozi wa taasisi hiyo Padre Godfrey Monjera amesema pamoja na jitihada wanazofanya kufanikisha miradi hiyo bado uhitaji wa huduma ya maji upo.
“Sisi kama taasisi ya kidini tumekuwa tukishughulika na miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya maji,lakini bila kushirikiana vizuri na serikali tusingeona matokeo mazuri” Padre Monjera amesema.
No comments:
Post a Comment