BAJETI YA WIZARA YA MAJI ILIYOSHEHENI VIPAUMBELE VYA KUBORESHA UPATIKANAJI WA MAJI 2025/26 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 8, 2025

BAJETI YA WIZARA YA MAJI ILIYOSHEHENI VIPAUMBELE VYA KUBORESHA UPATIKANAJI WA MAJI 2025/26



Na Okuly Julius _ DODOMA


Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso , akiwasilisha Mpango na Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2025/26, ameeleza vipaumbele vya Wizara vinavyolenga kuimarisha huduma za maji safi, usafi wa mazingira, na uendelevu wa rasilimali za maji nchini kote.

Katika hotuba yake, Waziri Aweso aeleza kuwa bajeti hiyo imelenga kujenga uwezo wa kitaasisi, kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji, na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa rasilimali za maji. Mpango huo umejikita katika maeneo yafuatayo:

Kipaombele cha kwanza ni Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji
Ambapo Aweso amesema Wizara hiyo itaweka mkazo katika kufanya tafiti na ufuatiliaji wa vyanzo vya maji vya juu na chini ya ardhi, kutangaza maeneo 141 kuwa maeneo tengefu, na kujenga vituo vipya 50 vya kuchunguza maji chini ya ardhi. Pia itaendelea kutoa vibali vya matumizi ya maji, kuimarisha jumuiya 271 za watumia maji, na kuendesha majukwaa ya kitaifa ya wadau wa sekta ya maji.

Kwa upande wa Huduma za Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini amesema katika mwaka wa fedha 2025/26, miradi 1,318 ya maji vijijini itatekelezwa, huku programu maalum ikiendelea kwa vijiji 1,781 ambavyo bado havijafikiwa na huduma. Upatikanaji wa maji vijijini unatarajiwa kuongezeka kutoka asilimia 83 hadi zaidi ya asilimia 85.

Aweso amesema kwa upande wa huduma za Maji Mijini
Wizara wizara hiyo imepanga kutekeleza miradi 225 ya maji mijini ikiwemo ujenzi wa mitandao ya maji katika Dar es Salaam, mradi wa Rufiji, na miradi ya maji na usafi wa mazingira katika miji kama Tunduma, Iringa, Ruangwa, Kigoma, na Mtwara-Mikindani. Dodoma pia imenufaika kwa miradi ya muda mfupi, wa kati na mrefu, ikiwemo mradi mkubwa kutoka Ziwa Victoria kupitia Singida.

Katika kudhibiti Upotevu wa Maji
Wizara imepanga kupunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 33.4 hadi kiwango cha kimataifa cha asilimia 20 kwa kufanya ukarabati wa miundombinu, kufunga mita za malipo kabla ya matumizi, na kuchukua hatua kali kwa waharibifu wa miundombinu ya maji.

Waziri Aweso ameeleza kuwa
Wizara hiyo itahakiki ubora wa maji kwenye vyanzo 2,200 na mifumo 8,245 ya usambazaji maji, sambamba na ujenzi wa maabara mpya Arusha na Tanga. Pia itaimarisha uwezo wa mamlaka za maji na CBWSOs kuhakikisha viwango vya kimataifa vinafikiwa na kudumishwa.

"Wizara itaendelea kuimarisha taasisi zake kwa kutoa mafunzo kwa watumishi, kuimarisha TEHAMA, na kuendeleza Chuo cha Maji. Pia, Mfuko wa Taifa wa Maji utaandaliwa kupata ithibati ya kufadhiliwa na Mifuko ya Mabadiliko ya Tabianchi,"

Na kuongeza kuwa "utekelezaji wa mpango huu utahakikisha maendeleo ya sekta ya maji yanaendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kumtua mama ndoo kichwani na kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora ya maji safi na salama," ameeleza Aweso


No comments:

Post a Comment