MHE.SIMBACHAWENE AWATAKA WAAJIRI KUGHARAMIA WATUMISHI KUSHIRIKI MKUTANO WA TRAMPA NA TAPSEA - OKULY BLOG

Breaking

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA | PIGA 0785 364 965

Tuesday, May 16, 2023

MHE.SIMBACHAWENE AWATAKA WAAJIRI KUGHARAMIA WATUMISHI KUSHIRIKI MKUTANO WA TRAMPA NA TAPSEA


Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,
amewataka Waajiri wote wa Taasisi za Umma kuwaruhusu na kuwagharamia Wanachama wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya kumbukumbu na Nyaraka Tanzani (TRUMPA) na Wanachama wa Chama Cha Makatibu Muhsusi (TAPSEA) kushiriki Mkutano wao.


Mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha washiriki zaidi ya elfu nane (8000) na utafanyika Visiwani Zanzibar kuanzia Mei 22 mpaka 27 ,2023 na Mgeni Rasmi katika Ufunguzi atakuwa Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 16,2023,Mtumba ,Jijini Dodoma,
Mhe.Simbachawene amesema kuwa Lengo la Mkutano huo ni kujadili majukumu mbalimbali ya kitaaluma ya wanachama wa vyama hivyo viwili ili kuleta ufanisi wa kada hiyo katika Sekta ya Umma.


"Kama mtakumbuka Novemba 27,2022 ,Mheshimiwa Rais wakati akifungua Mkutano wa Kumi wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA)uliofanyika Jijini Arusha alitoa maagizo kuwa ufanyike Mkutano Mkubwa kwa kuwaunganisha wanachama wa vyama vyote viwili yaani TRAMPA na TAPSEA tena akasema ufanyike Zanzibar na akaelekeza waajiri wawaachie wanachama hao kushiriki kwa wingi ili kujadili majukumu yao na umuhimu wa kada hiyo katika ustawi wa Utumishi wa Umma,"amesema Simbachawene


Mhe.Simbachawene amesema katika Mkutano huo Wanachama wote watakaohudhuria Watakula kiapo kwa ajili ya kutumikia nafasi zao lengo likiwa ni kuwaonesha na kuwakumbusha umuhimu wa kada hizo katika Utumishi wa Umma.


"Wote watakula kiapo ili waweze kutunza siri za Serikali katika taasisi zao na kusitokee kuvija kwa siri yeyote kwa namna yeyote ile ndio maana nazidi kuwakumbusha Waajiri kuhakikisha watumishi wao wanashiriki mkutano huo kwani ni muhimu kwa ustawi wa Taifa,"amesema Mhe.Simbachawene



Katika upande mwingine Mhe.Simbachawene amesema kila taasisi ina Mfumo wake wa Utunzaji kumbukumbu iwe ni umma au Binafsi ila lengo ni kulinda Maslahi ya taasisi yenyewe ndio maana Watunza Kumbukumbu na Makatibu Mahsusi ni viungo muhimu sana katika Ustawi wa Taasisi.

No comments:

Post a Comment

HABARI KUU KWA SASA

MREMBO WA CLUB KANIAMBUKIZA UGONJWA SUGU.

Naitwa Ally kutokea Dar es Salaam nchini Tanzania, ni kijana wa miaka 28 kwa sasa nikiwa nimeajiriwa katika shirika moja binafsi, katika mai...