DIRA ZA MAJI ZA MALIPO KABLA KUTOKOMEZA UBAMBIKIZAJI BILI ZA MAJI KWA WANANCHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 8, 2025

DIRA ZA MAJI ZA MALIPO KABLA KUTOKOMEZA UBAMBIKIZAJI BILI ZA MAJI KWA WANANCHI



Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akiwasilisha leo Mei 8,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026 .


Na Okuly Julius DODOM


WIZARA ya Maji imetaja mafanikio mbalimbali iliyoyapata katika mwaka wa fedha unaomalizika, ikiwemo kuanza kutumika kwa dira za maji za malipo kabla ya matumizi kwa wananchi na taasisi za umma, hatua iliyosaidia kuboresha huduma za maji na kupunguza malalamiko kuhusu ankara za matumizi.

Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb), akizungumza bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2025/26, ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya Shilingi trilioni 1.016 (Shilingi 1,016,894,958,000), ambapo Shilingi bilioni 73.77 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 943.11 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Katika maelezo yake, Waziri Aweso amesema mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na:

Kukamilika kwa ujenzi wa mabwawa 45 ya ukubwa wa kati na madogo kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kuboresha matumizi ya mifumo ya TEHAMA, hatua iliyoleta uwazi na uwajibikaji mkubwa katika ukusanyaji na matumizi ya mapato yatokanayo na huduma za maji.

Kuongeza udahili katika Chuo cha Maji kutoka wanafunzi 2,320 hadi 4,260, sawa na ongezeko la asilimia 84, sambamba na kufanya tafiti na kutoa machapisho ya kisayansi 52.

Kuanzisha Consultancy Bureau inayosaidia vijana wahitimu wa sekta ya maji kupata uzoefu wa kitaalamu, pamoja na Mfuko wa Taifa wa Maji kuendelea kuzisaidia taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kujenga uwezo wa kitaasisi.

Upatikanaji wa Dola za Marekani milioni 9.3 kupitia maandalizi ya maandiko ya miradi, kwa lengo la kuongeza vyanzo vya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini.

No comments:

Post a Comment