Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Johan Labuschagne (kushoto) akibadilishana mkataba na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyang’hwale, John Isack. John (kulia) ambapo mgodi utatoa kiasi cha shilingi bilioni 1.07 kutekeleza miradi ya CSR mwaka huu, wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Nyang’hwale, Ezekiel Ntiriyo na (katikati) ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Bi. Kaunga Omari na Afisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo (kushoto).
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Johan Labuschagne (kushoto) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Nyang’hwale, Ezekiel Ntiriyo,katika hafla hiyo ,katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyang’hwale, John Isack. John.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Johan Labuschagne akisaini mkataba
Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu na wageni wengine waalikwa katika hafla hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali.
Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya katika hafla hiyo
Wafanyakazi wa halmashauri hiyo wakifuatlia matukio wakati wa hafla hiyo.**
👉Mgodi kutoa shilingi bilioni 1.07 kwa utekelezaji wa miradi ya mwaka huuUwekezaji wa kampuni ya Barrick nchini yenye ubia Serikali nchini kupitia kampuni ya Twiga unazidi kuleta manufaa kwa wananchi ambapo mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo wilayani Msalala umesaini mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale ambapo katika kipindi cha mwaka huu utatoa kiasi cha shilingi bilioni 1 na milioni 75 za uwajibikaji kwa jamii (CSR) kwa ajili ya kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hafla ya kusaini mkataba huo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo umeshuhudiwa na viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyang’hwale, John Isack. John, amesema fedha hizo zitawezesha kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo baadhi yake ikiwa ujenzi wa madarasa manne katika Shule ya Mchepuo wa kingereza ya Kharumwa English Medium, Ukamilishaji wa stendi ya mabasi Ikangala na ununuzi wa madawati katika Shule za Msingi.
Miradi mingine ni ujenzi wa matundu ya vyoo 20 Shule ya Msingi Lubando, na Shule ya Msingi Gulumbai, ukamilishaji wa nyumba ya Mfanyakazi Zahanati ya Nyang’holongo,na ukamilishaji wa ununuzi wa gari la Wanafunzi katika Shule ya Mchepuo wa kingereza.
Pia, fedha hizo zitatumika kununua samani za zahanati kumi, ununuzi wa trekta, ukamilishaji wa madarasa mawili Shule ya Msingi Lushimba, Ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Msingi Kasubuya na Shule ya Msingi Mwamakiliga,ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Iyenze, kuanzisha Shule Shikizi ya Msingi Nyamikonze, kuchimba visima na uwekaji wa sola Zahanati ya Mwingiro na ukamilishaji wa darasa moja Shule ya Msingi Mwingiro.
John pia ametoa wito kwa madiwani na Watalamu wa Halmashauri hiyo kuwatangazia wananchi miradi hii inayotekelezwa na fedha za uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kutoka mgodi wa Barrick Bulyanhulu, ili wafahamu umuhimu wa kuwepo mgodi huu katika eneo lao “Hakikisheni mnafanya mikutano ya hadhara ya wananchi kwenye kata zenu kwa ajili ya kuongelea miradi ya CSR ili wananchi waelewe faida ya kuwa na mgodi huu”, amesisitiza.
Akizungumzia ufanisi wa miradi inayotekelezwa na fedha za CSR kutoka Barrick Bulyanhulu, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Nyang’hwale, Ezekiel Ntiriyo, amesema ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya CSR katika wilaya hiyo umekuwa ukizidi kuwa bora mwaka hadi mwaka na kwa sehemu kubwa utajikita kwenye miradi ya kijamii ambayo ni vipaumbele vya wananchi wa maeneo husika,
“Tunatekeleza mpango shirikishi, hatufanyi kama halmashauri - bila kupata mawazo ya wananchi na madiwani ambao ndio wawakilishi wao, na maelekezo ni kwamba mipango yote ijikite katika kutatua kero za wananchi na vipaumbele vyao,” amesema Ezekiel.
Kwa upande wake,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Johan Labuschagne, amesema kuwa mgodi wa Barrick Bulyanulu utaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha fedha za CSR zinazotolewa na mgodi huo kila mwaka zinaendelea kuwaletea maendeleo wananchi na kufanya maisha yao kuwa bora ili wanufaike na uwekezaji wa mgodi.
Naye Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Kaunga Omari, amewataka wataalamu na wahusika wote katika kufanikisha miradi iliyokusudiwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili ifikapo ili mwezi Desemba, 2025 miradi yote iwe imekamilika na ianze kutoa huduma kwa Wananchi.
No comments:
Post a Comment