MSAMAHA WA FAINI ZA MAJI WATANGAZWA BUNGENI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 8, 2025

MSAMAHA WA FAINI ZA MAJI WATANGAZWA BUNGENI


Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, akiwasilisha Bajeti ya Mageuzi ya Sekta ya Maji kwa mwaka wa fedha 2025/26, ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa mchango wao mkubwa katika kuisaidia Wizara kutekeleza majukumu yake, na kutangaza hatua muhimu zinazolenga kupunguza mzigo kwa wananchi na kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji nchini.

Akizungumza Bungeni, Waziri Aweso ameeleza kuwa maandalizi ya bajeti hiyo yamezingatia maoni na mapendekezo ya wananchi pamoja na wadau mbalimbali, jambo linaloonesha dhahiri ushirikiano kati ya Serikali na wananchi katika kujenga sekta bora ya maji.

Katika hatua ya kugusa moja kwa moja maisha ya wananchi, Waziri huyo ametoa salamu maalum kutoka Wizara ya Maji kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameridhia msamaha wa faini zote kwa wananchi wenye madeni ya maji katika Mamlaka mbalimbali.

Amesema, “Mama Samia amesamehe fine hizo, hivyo wafike kwenye Mamlaka kwa ajili ya utaratibu wa kurejeshwa huduma ya maji hadi tarehe 31 Mei 2025.”

Aidha, kwa wateja wote wenye madeni, Waziri Aweso amesisitiza kuwa ni fursa ya kipekee kwao kufika ofisi za Mamlaka za Maji kupewa utaratibu wa kulipa madeni hayo na kurejeshewa huduma mara moja bila usumbufu.

Katika hatua nyingine muhimu, Waziri Aweso ameagiza kuwa huduma ya maji isikatwe katika kipindi cha sikukuu au mwishoni mwa wiki. Pia ameelekeza kuwa maunganisho ya maji kwa wateja wapya yafanyike ndani ya siku saba, kwa mujibu wa miongozo ya Wizara.

No comments:

Post a Comment