WATAALAMU WA UJENZI WA MFUMO WA NeST WANOLEWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, May 13, 2025

WATAALAMU WA UJENZI WA MFUMO WA NeST WANOLEWA


Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) inaendelea kuboresha na kuongeza kasi ya matumizi ya teknolojia ili kuimarisha utendaji kazi katika maendeleo ya sekta ya Ununuzi wa Umma Nchini.

Akizungumza leo Mei 13, 2025 wakati akifungua mafunzo ya Usalama wa Mifumo ya TEHAMA Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Bw. Dennis Simba amesema, eneo la Ununuzi wa Umma ni eneo nyeti ambapo usalama wa taarifa zake zinazohifadhiwa ni kipaumbele kwa Serikali, na kwamba h ni muhimu Mifumo hiyo kuwa na Usalama wa kiwango cha juu.

“kutokana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na watu wenye nia ovu kutaka kupata taarifa zinazowanufaisha ni muhimu Usalama wa Mfumo tunaoujenga uwe wa kiwango cha juu na mafunzo haya yawafanye wataalam wetu waweze kuulinda Mfumo dhidi ya wale wote wenye nia Ovu. Amesema Simba

Aidha Mkurugenzi Simba ameongeza kuwa Mamlaka itaendelea kutekeleza maelekeo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wataalamu wanohusika na ujenzi na usimamizi wa mifumo, wanaendelea kujengewa uwezo ili kuweza kuendana na mabadiliko ya teknolojia yanayotokea siku hadi siku, ingawa wataalamu hao wana uwezo mkubwa wa kuendesha na kulinda usalama wa mifumo hiyo.

“Mamlaka tunaendelea kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais, hivyo niwatake washiriki wote wa mafunzo haya, kuhakikisha katika kipindi hiki cha wiki mbili munazingatia maelekezo ya wakufunzi na kuhakikisha munafanya mazoezi kwa vitendo ili kuweza kuongeza taaluma itakayowasaidia vilevile mumepata fursa ya kujifunza kwa nadharia na vitendo na Mamlaka itaendelea kuweka mazingira ya kuendelea kujifunza na kufanya mazoezi mara kwa mara.” Amesisitiza Mkurugenzi Simba 


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ujenzi wa Mfumo wa NeST Bw. Michael Moshiro amesema Mamlaka itahakikisha wataalamu hawa wanaopata mafunzo na wanakuwa na ujuzi madhubuti wa usalama wa mifumo ili kulinda taarifa za Serikali kwa manufaa ya Taifa.

“Kama munavyofahamu PPRA kwa kushirikiana na taasisi zingine za Serikali yetu tunajenga na kusimamia mfumo, na mfumo huu umejengwa na wataalamu wetu wa kitanzania, Aidha, tunafahamu kuwa teknolojia inakuwa kwa kasi nchini hivyo PPRA tumepokea maelekezo ya kuhakikisha wataalamu tunaowatumia wanapata mafunzo stahiki ambayo yataweza kuwasaidia kujenga mfumo lakini pia mfumo kuwa salama.”Amesema Bw. Moshiro.

Mafunzo hayo yanayohusisha Wataaalamu wa Ujenzi wa Mfumo wa ndani ya Mamlaka pamoja na Mtaalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu yanafanyika Jijini Arusha kwa muda wa siku 12 kabla ya kutamatika ifikapo tarehe 24 Mei, 2025.

No comments:

Post a Comment