WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo ,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 15,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Na.Alex Sonna_Dodoma
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Seleman Jafo amewataka watanzania kununua bidhaa zinazozalisha nchini ili kuviongezea nguvu Viwanda vya ndani na kuacha kununua vinavyotoka nje ya nchi.
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo leo Mei 15,2025,wakati akielezea mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita ambapo amesema kwa sasa Viwanda vimeongezeka hivyo watanzania wanatakiwa kuvipenda vitu vinavyozalishwa nchini ili kuviunga mkono Viwanda vya ndani.
"Niwaombe watanzania tununue bidhaa zinazozalishwa hapa kwetu tununue mabati yetu kwani tuna Viwanda vingi,"amesema Waziri Jafo.
Aidha,Waziri Jafo amesema Serikali itaendelea kujali Viwanda kwa kuhakikisha vinazidi kuongeza uzalishaji akitolea mfano Kiwanda cha utengenezaji wa mafriji Jijini Arusha.
"Kwa mara ya kwanza ukienda Arusha utakutana na mafriji ya kisasa ya kuweka maiti sita,bei yake ni nafuu,tunataka kujali vya kwetu kwa kiwango kubwa,"amesema Waziri Jafo.
No comments:
Post a Comment