WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YATAJA MAFANIKIO MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 14, 2025

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YATAJA MAFANIKIO MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA



Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akiwasilisha leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akiwasilisha leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akiwasilisha leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.


Na.Alex Sonna-DODOMA


Wizara ya Viwand ana Biashara imepata mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo uendelezaji wa miradi ya kielezo na kimkakati; upanuzi na ujenzi wa viwanda; uendelezaji wa teknolojia mbalimbali; atamizi na ubunifu; utafutaji wa masoko ya bidhaa za Tanzania ndani na nje ya nchi; ubora wa bidhaa na ushindani wa kibiashara; na utatuzi wa migogoro.

Mafanikio hayo yametajwa leo Mei 14,2025 bungeni na Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Selemani Jafo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Waziri Jafo amesema Serikali imefanikiwa kulipa fidia ya shilingi bilioni 15.4 kwa wananchi 1,142 wanaopisha utekelezaji wa Mradi Unganishi wa Mchuchuma na Liganga.

Pia imeendelea kutekeleza miradi wa Magadi Soda Engaruka, Kufufua Kiwanda cha Kilimanjaro Mashine Tools (KMTC), Kiwanda cha Bidhaa za Kibailojia (TBPL).

Waziri Jafo amesema Katika kipindi cha miaka minne Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuvutia uwekezaji wa viwanda nchini ambapo Kupitia juhudi hizo viwanda vikubwa vimejengwa na kupanuliwa vikiwemo Kiwanda cha Wild Flower and Grains Ltd; Kiwanda cha Chokaa cha Maweni (Huaxin Cement Co Ltd).

Pia Viwanda vya kuunganisha magari (Kiwanda cha GF Trucks and Equipment Ltd na Kiwanda cha Saturn Corporation Limited); Kiwanda cha kutengeneza vioo (Sapphire Float Glass (Tanzania) Company Limited); Kiwanda cha Sukari cha Kilombero; Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi na Kiwanda cha Sukari Kagera.
Waziri Jafo amesema Serikali katika kuhakikisha inapunguza utegemezi wa uagizaji wa vifaa tiba nchini, Wizara kupitia Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo (TEMDO) imefanikiwa kupata ithibati inayoruhusu kusanifu na kutengeneza vifaa tiba mbalimbali.

No comments:

Post a Comment