
Aliyekuwa Naibu Katibu MKUU Wizara ya Elimu Dkt. Charles Mahera (Kushoto) , akimkabidhi rasmi ofisi Naibu Katibu Mkuu mpya, Dkt. Hussein Mohamed Omar(kulia) , ambaye ameripoti kazini kufuatia uteuzi wake na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Makabidhiano hayo yamefanyika Juni 27, 2025 Jijini Dodoma na kushuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, leo Juni 27, 2025 amempokea rasmi Naibu Katibu Mkuu mpya anayeshughulikia Elimu, Dkt. Hussein Mohamed Omar, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Katika hotuba yake ya kumkaribisha, Prof. Nombo alieleza kuwa Wizara inaendelea kutekeleza mageuzi makubwa ya elimu yanayolenga kutoa stadi, maarifa, na ujuzi kwa Watanzania. Alimhakikishia Dkt. Omar ushirikiano wa karibu katika kuhakikisha dira hiyo inatekelezwa kikamilifu.

Kwa upande wake, Dkt. Omar alitoa shukrani kwa mapokezi mazuri aliyoyapata kutoka kwa watumishi wa Wizara, na akasisitiza kuwa yupo tayari kuwajibika ipasavyo katika kuendeleza mageuzi ya elimu katika nyanja zote.













No comments:
Post a Comment