Na Hamida Ramadhan
NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile, amesema kuwa miradi yoyote ya maendeleo inayosimamiwa na Serikali haitafika mwisho iwapo itakumbwa na mianya ya rushwa, akisisitiza kuwa nidhamu ya matumizi ya fedha ni msingi wa mafanikio ya sekta hiyo.
Akizungumza Juni 18, 2025 katika banda la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma, Mhe. Kihenzile alisema kuwa rushwa si tu inachelewesha utekelezaji wa miradi bali pia huua matumaini ya wananchi.
"Rushwa katika miradi ya maendeleo ni kikwazo kikubwa. Haitakiwi kuvumiliwa hata kidogo. Tunahitaji TAKUKURU kuimarisha usimamizi hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ili kuhakikisha tunapata viongozi waadilifu na wa kizalendo,” alisema kwa msisitizo.
Aidha, Mhe. Kihenzile amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa miradi ya uchukuzi inatekelezwa kwa viwango vya hali ya juu na kwa manufaa ya wananchi. Alisisitiza kuwa mafanikio ya sekta hiyo yanategemea usimamizi thabiti na mapambano ya kweli dhidi ya rushwa.
"Niitake TAKUKURU na wadau wengine wa usimamizi wa miradi kuhakikisha kuwa fedha za umma zinalindwa kwa nguvu zote, hasa katika kipindi hiki nyeti cha kuelekea uchaguzi mkuu,” aliongeza.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yameendelea kuwa jukwaa muhimu la Serikali kuwasiliana moja kwa moja na wananchi, kusikiliza kero, kutoa elimu ya sera na kusisitiza uwajibikaji kwa taasisi zake.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Uelimishaji Umma wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Faustine Malecha, alisema kuwa taasisi hiyo itaendelea kutumia jukwaa hilo kutoa elimu kuhusu madhara ya rushwa na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika uchaguzi kwa njia za uadilifu.
"TAKUKURU tumekuja hapa kutoa elimu kuhusu madhara ya kutoa na kupokea rushwa. Tunawahamasisha wananchi kuhakikisha hawachagui viongozi wanaonunua nafasi kwa rushwa, kwani viongozi wa aina hiyo hawawezi kuleta maendeleo ya kweli,” alisema Malecha.

No comments:
Post a Comment