MAJALIWA: MAPINDUZI MAKUBWA YAMEFANYIKA KATIKA SEKTA YA MICHEZO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 2, 2025

MAJALIWA: MAPINDUZI MAKUBWA YAMEFANYIKA KATIKA SEKTA YA MICHEZO


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya michezo kama sehemu ya utekelezaji wa Ibara ya 243 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020.

Pia, Waziri Mkuu ametaja mafanikio yaliyopatika katika sekta ya michezo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka shilingi bilioni 285 mwaka 2024/2025 hadi bilioni 519 katika mwaka wa fedha 2025/2026. “Ongezeko hili ni kubwa zaidi katika historia ya Wizara hii.”


"Serikali imeendelea na mkakati wake wa kuhakikisha inainua michezo hapa nchini, kila mmoja kwa nafasi yake uwe mchezaji, wakala, mdhamini endelezeni taaluma hiyo. Leo hii tuna kila sababu ya kumpongeza na kumshukuru rais wetu kwa kufungua hiyo milango na kuongeza bajeti na kuruhusu sekta binafsi kushiriki kwenye michezo.”
 
Ameyasema hayo jana usiku (Jumapili, Juni Mosi, 2025) katika hafla ya usiku wa tuzo zilizoandaliwa na Baraza la Michezo Tanzania kwa wanamichezo waliofanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa iliyofanyika katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment