RAIS SAMIA KUKAGUA RING ROAD, UWANJA WA NDEGE MSALATO KESHO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 13, 2025

RAIS SAMIA KUKAGUA RING ROAD, UWANJA WA NDEGE MSALATO KESHO.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 14, Juni 2025 atakagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mzunguko wa nje wa Dodoma (outer ring roads) Km 112 na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato.

Katika ziara hiyo, Dkt. Samia ataambatana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bw. Akinwumi Adesina.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema ziara hiyo itakayoanzia eneo la Mtumba-Veyula - Msalato itahitimishiwa kwa Rais Dkt. Samia kuzungumza na wananchi katika eneo la Nala na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia utekelezaji wa miradi mikubwa na ya kimkakati inayoendelea mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment