TANROADS WAPATA TUZO YA UHIFADHI MAZINGIRA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 5, 2025

TANROADS WAPATA TUZO YA UHIFADHI MAZINGIRA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philipo Mpango (kushoto) akikabidhi tuzo ya Uhifadhi wa Mazingira, Bi Zafarani Madayi, Meneja wa Mazingira na Jamii wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, ambayo kitaifa leo yamefanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma

Mkuu wa mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa maafisa wa wizara ya ujenzi leo alipotembelea banda la maonesho la wizara hiyo pamoja na wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira Duniani, ambapo kitaifa yamefanyika kwenye viwanja vya Kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma

Baadhi ya Watumishi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) wakiwa na tuzo waliyopata leo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani. Aliyeshika tuzo hiyo ya uhifadhi wa mazingira ni Meneja wa Mazingira na Jamii wa taasisi Bi. Zafarani Madayi





Na Mwandishi Wetu, Dodoma


Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), leo tarehe 05 Juni, 2025 imepata tuzo ya Uhifadhi wa Mazingira katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira iliyofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Tuzo hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillipo Mpango, kutokana na mchango wake wa utunzaji mazingira hususan katika utekelezaji wa ujenzi wa barabara za juu (Fly Over) na mradi wa ujenzi wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT) ambayo imetajwa kuwa na mchango mkubwa katika kupunguza gesijoto nchini.

Dkt. Mpango ameelekeza Wizara, Taasisi na Mamlaka zote za Serikali kuhamasisha na kuelimisha jamii umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kupunguza gesijoto nchini.

Katika hotuba yake wakati akiadhimisha Siku ya mazingira Duniani iliyofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma leo Juni 5, 2025 Dkt. Mpango amesema kuwa jamii inapaswa kupewa elimu

No comments:

Post a Comment