TANZANIA MWENYEJI TUZO ZA UTALII DUNIANI KWA MWAKA 2026 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, June 29, 2025

TANZANIA MWENYEJI TUZO ZA UTALII DUNIANI KWA MWAKA 2026



Baada ya kuandaa kwa mafanikio makubwa Tuzo za Utalii za Dunia (World Travel Awards) Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi , Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo ngazi ya dunia mwaka 2026.

Uamuzi huo umetangazwa rasmi na Rais wa Tuzo hizo, Graham Cooke kwenye hafla ya 32 ya Utoaji Tuzo za Utalii Duniani zilizofanyika Johari Rotana jijini Dar es salaam tarehe 28.06.2025.

Akitoa Tangazo hilo Graham amepongeza juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali ya Tanzania katika kukuza sekta ya utalii nchini.

Hafla ya Utoaji Tuzo za Utalii kwa Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi imeacha alama kubwa ya kitaifa na kimataifa, ambapo Tanzania ilionyesha uwezo wa hali ya juu katika maandalizi, mapokezi na ugeni, ukarimu na ubunifu.

Graham Cooke ameeleza kuwa mazingira mazuri, ukarimu wa Watanzania, na uwepo wa vivutio vya kipekee vya utalii vimeifanya Tanzania kuwa chaguo bora kwa tukio la ngazi ya juu kabisa duniani katika sekta ya utalii.

Tukio la mwaka 2026 linatarajiwa kuvutia wadau wa utalii kutoka mataifa mengi zaidi na kuchochea ukuaji wa sekta hiyo nchini.




No comments:

Post a Comment