TANZANIA NA RWANDA KUSHIRIKIANA KATIKA UJENZI WA MIUNDOMBINU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, June 22, 2025

TANZANIA NA RWANDA KUSHIRIKIANA KATIKA UJENZI WA MIUNDOMBINU



Kigali-Rwanda


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Wakala ya Maendeleo ya Usafirishaji Rwanda (Rwanda Transport Development Agency-RTDA) zimekubaliana kushirikiana katika nyanja mbalimbali hususani katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Hayo yamejiri mjini Kigali wakati Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff akiwa ameambatana na wataalamu wengine kutoka Wakala huo, Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambao wapo nchini Rwanda kwa ziara ya kikazi.

Katika ziara hiyo wataalamu hao wameweza kubaini nyanja mbalimbali za kushirikiana hususan katika ujenzi wa miundombinu ya barabara ikiwemo barabara za mawe(Corbal stone roads) na ujenzi wa madaraja ya kitefutefu (suspension and suspended bridge) ambapo Rwanda yanatekelezwa na shirika la 'Bridges to prosperity' (B2P).

Madaraja hayo hutumikia zaidi kurejesha mawasiliano kwa haraka na kwa gharama nafuu zaidi pindi kunapotokea uharibifu wa madaraja yapitayo magari hasa kipindi cha masika na maeneo ambayo jamii zimetengwa na mito mikubwa ukilinganisha na gharama za ujenzi wa daraja la kupitisha magari kuonekana kuwa kubwa sana kwa kipindi hicho.



No comments:

Post a Comment