TCDC YADHAMIRIA KUIMARISHA VYAMA VYA USHIRIKA KWA KUTOA MAFUNZO YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 6, 2025

TCDC YADHAMIRIA KUIMARISHA VYAMA VYA USHIRIKA KWA KUTOA MAFUNZO YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI

AFISA Ushirika Mwandamizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC),Happiness Olotu,akizungumza na wanaushirika wa Haydom AMCOS kilichopo Haydom wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025.

Na.Alex Sonna-MANYARA

KATIKA kuunga mkono juhudi za kuinua sekta ya kilimo nchini, Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imefanya mafunzo mahsusi kwa vyama vya ushirika mkoani Manyara, kwa lengo la kubadilisha kilimo kuwa cha kibiashara na kuongeza kipato cha wakulima wa mazao ya mbogamboga na bustani.

Afisa Ushirika Mwandamizi kutoka TCDC, Happiness Olotu, ameyasema hayo wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025.

Olotu amesema kuwa mafunzo hayo yamefanyika katika wilaya ya Simanjiro, chama cha AMCOS Mirerani kilichopo Mererani, na wilaya ya Mbulu, vyama vya msingi Gidesha AMCOS na Haydom AMCOS vinavyoshughulika na mazao ya mbogamboga.

Amesema mafunzo hayo yamegusa masuala ya uzalishaji wa kisasa, uongezaji thamani wa mazao, matumizi bora ya rasilimali ardhi pamoja na uelewa wa masoko, hatua inayolenga kuimarisha uwezo wa wakulima kuingia kwenye ushindani wa soko la kitaifa na kimataifa.

“Tunataka kuona vyama vya ushirika vikigeuka kuwa daraja la maendeleo kwa wakulima, si tu kwa uzalishaji bora, bali pia kwa kuwaunganisha na wadau wa masoko na mitaji,” amesema Olotu.

Olotu amesema ushirikiano kati ya Maafisa Ushirika na Maafisa ugani katika maeneo husika ni muhimu kwa kuhakikisha wakulima wanafuatiliwa, wanashauriwa na wanasaidiwa katika hatua zote za utekelezaji wa maarifa waliyopewa.

Aidha, amewataka wanachama wa vyama vya ushirika vilivyonufaika kutambua nafasi yao katika kuleta mabadiliko, wakitumia ujuzi walioupata kubadilisha maisha yao na jamii zao, huku akiwahakikishia usaidizi kutoka Tume iwapo watakutana na changamoto.

Kwa mujibu wa Tume, jitihada hizi ni sehemu ya mkakati mpana wa kitaifa wa kuimarisha mfumo wa ushirika nchini, kwa kulifanya kuwa chombo imara cha kuinua wakulima wadogo kiuchumi na kuchochea maendeleo endelevu ya vijijini.

Kwa upande wake Afisa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Bahati Majaliwa, amesema Wizara ya Kilimo inaendelea kuimarisha sekta ya ushirika kwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara wanachama wa vyama vya ushirika nchini ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi kupitia uzalishaji wa mazao kwa tija na kwa kuzingatia mahitaji ya soko.

AFISA Ushirika Mwandamizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC),Happiness Olotu,akizungumza na wanaushirika wa Haydom AMCOS kilichopo Haydom wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025.

AFISA Ushirika Mwandamizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC),Happiness Olotu,akizungumza na wanaushirika wa Haydom AMCOS kilichopo Haydom wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025.

AFISA Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Dominick Nzimba,akizungumza na wanaushirika wa Haydom AMCOS kilichopo Haydom wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025.

MWENYEKITI wa Haydom AMCOS Bw.John Sanka,akizungumza wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 yaliyofanyika katika Haydom AMCOS kilichopo Haydom wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara

SEHEMU ya Wanaushirika wa Haydom AMCOS wakifatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 yaliyofanyika Haydom AMCOS kilichopo Haydom wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara

MHADHIRI MoCU CPA Msongore Alex,akiwasilisha mada kwa wanaushirika wa Haydom AMCOS kilichopo Haydom wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025.

AFISA Ushirika Mwandamizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC),Happiness Olotu (wa pili kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025.

No comments:

Post a Comment