WAZIRI CHANA ATETA NA UJUMBE KUTOKA BENKI YA DUNIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 14, 2025

WAZIRI CHANA ATETA NA UJUMBE KUTOKA BENKI YA DUNIA



Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Nathan Belete mara baada ya kumalizika kwa warsha ya kujadili masuala ya uhifadhi na Mchango wake katika Utalii na Maendeleo ya Jamii jijini Arusha leo Juni 14,2025.

Lengo la kikao hicho ni kujadiliana namna bora ya kukuza mashirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Benki ya Dunia katika kuendeleza miradi ya kimkakati kwenye Sekta ya Maliasili na Utalii kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii (anayeshughulikia Maliasili),Kamishna Benedict Wakulyamba, Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS),Prof. Dos Santos Silayo na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru.



No comments:

Post a Comment