"𝘾𝙝𝙖𝙢𝙖 𝘾𝙝𝙖 𝙈𝙖𝙥𝙞𝙣𝙙𝙪𝙯𝙞 (𝘾𝘾𝙈) 𝙠𝙞𝙢𝙚𝙞𝙩𝙖 𝙢𝙠𝙪𝙩𝙖𝙣𝙤 𝙈𝙠𝙪𝙪 𝙈𝙖𝙖𝙡𝙪𝙢 𝙨𝙞𝙠𝙪 𝙮𝙖 𝙠𝙚𝙨𝙝𝙤 𝙅𝙪𝙢𝙖𝙢𝙤𝙨𝙞 𝙩𝙖𝙧𝙚𝙝𝙚 26 𝙅𝙪𝙡𝙖𝙞 2025"
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, 𝗖𝗣𝗔. 𝗔𝗺𝗼𝘀 𝗠𝗮𝗸𝗮𝗹𝗹𝗮 wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa lengo la mkutano huo ni kufanya marekebisho madogo ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.
CPA. Makalla amesema kuwa Mkutano huo utafanyika kwa njia ya mtandao na tayari maandalizi yote yamekamilika.
"Nimepokea simu nyingi kutoka kwa watu na kwenye mitandao watu wameandika mambo mengi, nawathibitishia kuwa kesho tutakuwa na mkutano Mkuu Maalumu ambao utafanyika kwa njia ya mtandao," Amesema CPA.
No comments:
Post a Comment