Dkt. Kilabuko: Ushirikiano wa kikanda muhimu kukabili maafa ya kibinadamu - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 10, 2025

Dkt. Kilabuko: Ushirikiano wa kikanda muhimu kukabili maafa ya kibinadamu


Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. James Kilabuko amehimiza ushirikiano wa kikanda katika kukabiliana na majanga ya kibinadamu yanayochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kuimarisha vituo vya ufuatiliaji wa majanga na tahadhari ya mapema (Situation Room).

Akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya kubadilishana uzoefu, yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na UNDRR na Kituo cha Sayansi cha Afrika Magharibi kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (WASCAL), Dkt. Kilabuko alisema mafunzo hayo ni sehemu ya kuimarisha uwezo wa kanda katika kukabili matukio ya majanga. Mafunzo hayo yalihusisha ujumbe kutoka Ghana, Togo na Burkina Faso.

Dkt. Kilabuko alieleza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa majanga, kupitia vituo vyenye uwezo wa kukusanya taarifa mbalimbali, zikiwemo za hali ya hewa, maji, kijamii na kiuchumi, jambo linalosaidia kukabili majanga kama vile ukame na mafuriko.

“Tunauzoefu mkubwa wa kiutendaji ambao unasaidia kuhakikisha vituo vyetu vinafanya kazi kwa ufanisi kwa kuratibu taasisi mbalimbali kukabiliana na majanga,” alisema Dkt. Kilabuko.





No comments:

Post a Comment