
NA. MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chombo kinachosimamia utekelezaji wa Programu zinazofadhiliwa na Mfuko wa Dunia (Tanzania National Coordinating Mechanism - TNCM) Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha wajumbe wa chombo hicho kwa ajili ya kupitisha Maboresho ya Bajeti ya Utekelezaji wa Programu za Malaria, Kifua Kikuu, UKIMWI ambayo ni mzunguko wa saba (GC7) kwa mwaka 2024 hadi 2026.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 10 Julai, 2025 katika Jengo la Tume ya Ushindani Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI, Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Medical Stores Department (MSD), Local Fund Agent (LFA), Sekretarieti ya TNCM, Asasi za Kiraia (Non State Actors - NSAs), Mashirika ya Kimataifa (WHO, UNAIDS), Wadau wa Maendeleo (US Government, British High Commission pamoja na wawakilishi kutoka Mfuko wa Dunia).








No comments:
Post a Comment