MAAFISA MAENDELEO YA JAMII FURUKUTENI KUTOA ELIMU YA UNUNUZI WA UMMA WA ASILIMIA 30 - MDEMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, July 11, 2025

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII FURUKUTENI KUTOA ELIMU YA UNUNUZI WA UMMA WA ASILIMIA 30 - MDEMU


‎Na WMJJWM - IRINGA

‎Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kuboresha utendaji wao wa kazi kwa kwa kuwa sekta hiyo ni mtambuka na inagusa jamii katika kila nyanja.
‎Ametoa wito huo wakati akifungua mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhusu ushiriki wa makundi Maalum katika  ununuzi wa zabuni za umma wa asilimia 30 ya, mkoani Iringa.
‎Amesema  Maafisa Maendeleo ya Jamii kuwaelimisha wananchi kuhusu ununuzi wa umma na kuwahamasisha kutumia fursa ya hisa ya asilimia 30, Pamoja na usajili wa vikundi vya makundi maalum ili viweze kushiriki kikamilifu na kunufaika na fursa hiyo.
‎"Maafisa Maendeleo ya Jamii mnapaswa kuwa mstari wa mbele; sekta hii ni mtambuka na ina nafasi kubwa katika kubadilisha maisha ya wananchi. Tusiache makundi maalum nyuma, tuwape elimu na kuwaongoza kushiriki kikamilifu katika fursa zilizopo."
‎Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa,. Venance Ndiyagundula, ameishukuru Serikali kwa kutoa mafunzo hayo, akisisitiza kuwa yatawasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi. Ameahidi kuwa Mkoa wa Iringa utaendelea kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa mafunzo hayo ili kufanikisha malengo ya Serikali. ‎
‎Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Juliana Kibonde, amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Maafisa Maendeleo ya Jamii ili waweze kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi, kupata  elimu ya ujasiriamali na kusaidia vikundi hivyo kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.
‎Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii walioshiriki wameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwapatia mafunzo hayo, na kuahidi kutekeleza kwa ufasaha kwa maslahi ya maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment