NI WAKATI WA SIASA ZENYE TIJA - DORIS CORNEL - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 26, 2025

NI WAKATI WA SIASA ZENYE TIJA - DORIS CORNEL



Katika kile kinachoonekana kama msimamo thabiti na wa maamuzi, mmoja wa Kada wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambaye amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM) Doris Cornel Maarufu Doreen Don ameibuka na kutoa kauli nzito kuhusu mwelekeo wa siasa nchini, akisisitiza umuhimu wa kufanya siasa zenye tija badala ya siasa za msimu na ajenda hewa.

Kupitia ujumbe wake uliojaa uzito wa kisiasa na kiitikadi, kiongozi huyo amesema “Ni wakati wa kufanya siasa zenye tija, hatuwezi kufanya siasa zenye ajenda ya kiupepo upepo. Kama ni mabadiliko, yatatoka ndani ya CCM yenyewe.”

Amesema wapo watu ambao furaha yao kuu ni kuwa wapinzani tu wa kila jambo, bila kuzingatia maslahi mapana ya taifa.

Ameeleza kuwa baadhi ya watu hao wanatafuta umaarufu kwa kuibua ajenda zisizo na mwelekeo, huku wakipotezea umma muda na fursa ya kujadili maendeleo ya kweli.

“Haiwezekani kuwa ndani ya chama halafu kila wakati ni ajenda za msimu. Mara hiki, kesho kimepita, wameibuka na jambo jingine kabla hata ya kuona matokeo. Hakuna consistency. Huku ni kuwahadaa Watanzania ambao wanahitaji maendeleo, si maigizo ya kisiasa.”

Aidha, kiongozi huyo amesema ameweka bayana msimamo wake wa kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wanachama wengine wa chama hicho katika kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kwa amani, mshikamano na maendeleo ya kweli.

“Mimi binafsi nimeamua kuungana na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wana CCM wengine kuhakikisha taifa hili linasonga mbele. I'm so happy nimetua mzigo leo wa matusi, kejeli, mitafaruku isiyo na maana.”

Katika ujumbe huo uliogusa hisia za wengi, kiongozi huyo alisisitiza kuwa hatua hiyo haijatokana na woga au kutafuta sifa, bali ni kwa ajili ya dhamira ya moyo wake na wito wa kuchangia mustakabali wa taifa kwa njia chanya.

“From now on, I call it past and I leave with no regret. Not out of fear, nor for applause but for my heart and for the cause. Let the history write what it must. I'm walking ahead in faith and joy.”

Kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti mitandaoni, huku baadhi ya wachambuzi wa siasa wakieleza kuwa ni mfano wa aina ya uongozi unaojali matokeo kuliko malumbano.
"Viva Tanzania, Viva CCM!"

No comments:

Post a Comment