Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa l tarehe 13 Julai, 2025 amemkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati, Bi Neema Chalila Mbuja tuzo ya umahiri kufuatia mchango wake alioutoa wakati wa Maonesho ya Dunia ya Biashara ya Osaka nchini Japan kwa upande wa Mawasiliano na kuitangaza nchi.
Mhe Majaliwa amempongeza Bi. Mbuja wakati wa kilele cha Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba 2025.
Sambamba na hilo Mhe Majaliwa amempongeza Bi. Mbuja kwa kuwa muongozaji wa shughuli na kuwa mahiri wakati wa Kongamano la Kimataifa la Biashara, Uwekezaji na Utalii kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025.
Kwa upande wake Bi. Mbuja amemshukuru Mhe. Majaliwa kwa kukabidhi tuzo hiyo iliyotolewa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara TANTRADE na kuahidi kuendelea kuitangaza Wizara ya Nishati Kimataifa.
No comments:
Post a Comment