
1. Afya kwa Wote
• Kuzindua Mfumo wa Taifa wa Bima ya Afya kwa Wote (Wazee, Watoto, Wajawazito na Walemavu).
• Serikali kugharamia vipimo na matibabu ya kibingwa kwa 100% kwa wasiojiweza kwenye magonjwa makuu kama Saratani, Figo, Moyo, Kisukari na Mifupa.
• Kuajiri wahudumu wa afya 5,000 (Wauguzi na Wakunga).
• Kutoa marufuku kwa hospitali zote nchini kuzuia miili ya marehemu kuchukuliwa na ndugu zao.
2. Elimu Bora na Sayansi
• Kuanzisha mkakati wa kisayansi kuhakikisha wanafunzi wa darasa la tatu wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu.
• Kuajiri walimu 7,000 wa Hisabati na Sayansi.
• Kuanzisha mpango wa pamoja kati ya waajiri, VETA na vyuo vikuu ili kulinganisha mafunzo na sekta za kipaumbele.
3. Vijana na Uchumi
• Kutoa TZS Bilioni 200 kwa ajili ya mitaji kwa vijana na kurasimisha sekta zisizo rasmi.
4. Viwanda na Uwekezaji
• Kuanzisha programu ya ujenzi wa mitaa ya viwanda katika wilaya mbalimbali.
5. Maji na Miundombinu ya Kijamii
• Kujenga Gridi ya Taifa ya Maji (kwa matumizi ya nyumbani, kilimo na biashara) kutoka Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa na mito mikubwa.
6. Nishati Safi
• Kuendeleza matumizi ya nishati safi ya kupikia.
7. Uwajibikaji wa Viongozi
• Kuweka mifumo rasmi ya uwajibikaji kwa Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Watendaji wengine wa serikali ili kujibu maswali ya wananchi kwa njia ya kidijitali na SMS.
8. Demokrasia na Ushirikishwaji
• Kuendeleza mashauriano na wadau wa siasa, taasisi za kiraia na sekta binafsi kwa kuunda tume ya kuanzisha mazungumzo ya maridhiano na upatanishi, na kuandaa mazingira ya kuanza mchakato wa Katiba Mpya.
9. Miaka Mitano Ijayo
• Kuendelea kuboresha miundombinu na kusimamia haki, amani na utulivu wa kisiasa ili kukuza uchumi, kuleta maendeleo na ustawi wa nchi.
10. Jamii ya Kazi na Maendeleo
• Kujenga jamii ambapo miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na inaleta matokeo kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment