DKT. BITEKO AOMBA KURA YA NDIYO KWA WAJUMBE BUKOMBE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, August 2, 2025

DKT. BITEKO AOMBA KURA YA NDIYO KWA WAJUMBE BUKOMBE



Mbunge wa Jimbo la Bukombe anayemaliza muda wake, Dkt. Doto Mashaka Biteko ambaye ameomba tena ridhaa ya kutetea kiti hicho, ameeleza furaha na shukrani aliyonayo kwa Wananchi wa Bukombe kufuatia ushirikiano waliompa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Dkt. Biteko amesema hayo Agosti 2, 2025 kwa nyakati tofauti wakati akiomba kura kwa wajumbe wa Chama cha Mapinduzi wa Kata za Lyambamgongo, Uyovu, Bugelenga, Katome, Igulwa na Runzewe Mashariki zilizopo katika Jimbo la Bukombe.


" Mimi na viongozi wenzangu wakiwemo wa vijiji na madiwani ukianzia sekta ya Nishati tumesambaza umeme kila mahali, Sekta ya miundombinu tumeongeza mtandao wa barabara kutoka km 259 hadi km 1,445 na Sekta ya Elimu tunaongoza kwa kuwa na shule nyingi za Msingi na Sekondari tofauti na ilivyokuwa Mwaka 2015 hatukuwa na shule ya sekondari ya upili hata moja lakini mwaka 2025 tunazo shule TANO, Kwa upande wa sekta ya afya tumepata miradi mbalimbali na fedha nyingi za kuboresha huduma za afya katika wilaya yetu ya Bukombe”.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa dhamira yake kwa Wanabukombe ni Maendeleo na wakati wote anafikiria kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa Wananchi wote "Moyoni mwangu ninalo deni kubwa sana la kufanya kazi zaidi kutokana na heshima ambayo wananchi wameendelea kunipa wakati wote”.


No comments:

Post a Comment