EDWARD OLE LEKAITA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KITETO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 26, 2025

EDWARD OLE LEKAITA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KITETO



Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mkoani Manyara mwaka 2020 hadi 2025 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wakili Edward Ole Lekaita amechukua rasmi fomu ya uteuzi kugombea Ubunge wa Jimbo la Kiteto kwa ajili ya kuipeperusha bendera ya Chama Hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Zoezi hilo limefanyika katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara mara baada ya Wakili Ole Lekaita kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM kuwa mgombea wa chama hicho katika Jimbo la Kiteto.

Wakili Ole Lekaita amesindikizwa na viongozi mbalimbali wa chama kutoka Wilaya ya Kiteto, watia nia wenzake na wanachama wa CCM kuanzia Ofisi ya CCM Mkoa, Ofisi ya CCM Wilaya, Ofisi za CCM za Kata na matawi, Viongozi wa dini na kumalizia matembezi yake katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hizo amewashukuru wajumbe kwa kumchagua kwa kishindo katika kata zote kwa kupata kura 12,532 akiwa ni mshindi wa pili kwa wingi wa kura nchi nzima ambapo aliyeongoza ni Bi Judith Kapinga mgombea ubunge jimbo la Mbinga Vijijini aliyepata kura 12,900.

"Wanachama wenzangu hili ni deni kubwa la kuongeza chachu ya maendeleo endelevu ambayo kwa kipindi cha miaka mitano yamefanyika kupitia serikali yetu inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambayo yamefanyika kwa wingi ukilinganisha na matarajio ya wananchi" Amekaririwa

Awali Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kiteto Ally Issa Kichuri amemtaka Wakili Ole Lekaita kusoma kwa umakini Fomu hizo na kuzirejesha kabla ya Tarehe 27 katika Ofisi hizo na kuheshimu kanuni za kimaadili Kuelekea katika uchaguzi Mkuu wa Octoba 2025.

Naye, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kiteto Ndg Hassan Losioki amewataka wagombea walioshindwa na ambao hawakuteuliwa na chama kuacha makundi ya uchaguzi na badala yake kuwaunga mkono wagombea walioteuliwa na CCM kupeperusha bendera katika uchaguzi Mkuu.







No comments:

Post a Comment