Na Mwandishi Wetu, Handeni
HALMASHAURI ya Mji Handeni, mkoani Tanga, imetoa wito kwa wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika mradi wa kuchakata mawe na kokoto ili kuongeza mapato ya ndani na kuchochea maendeleo ya halmashauri hiyo.
Akizungumza Agosti 12, 2025 katika ziara ya kukagua mradi huo uliopo milima ya madini ya mawe ya Kwedihegwa na Kwaluhizo Kata ya Kideleko mjini humo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Maryam Ukwaju, amesema mradi huo unatarajiwa kuwa chanzo kipya cha mapato ambacho kitatoa ajira kwa wananchi wa maeneo jirani, sambamba na kuchangia utekelezaji wa miradi ya kijamii.
“Niagize Idara ya viwanda, biashara na uwekezaji harakisheni kukamilisha taratibu zote muhimu na kuweka mazingira wezeshi na taratibu za kupata mbia zitafanyika kwa kutumia mifumo ya ununuzi wa umma kwa kushirikiana Kituo cha uwekezaji kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP Center),”amesema.
Awali, akitoa taarifa ya mradi huo, Mkuu wa Idara ya Viwanda, Biashara, Danson Mongi, amesema mchakato wa kuwekeza katika milima hiyo uliidhinishwa katika vikao vya kamati ya fedha na utawala na kuidhinishwa na Baraza la Madiwani Mei 8, 2025.
Amesema hadi sasa Halmashauri ya Mji imelipia leseni za uchimbaji mdogo ambazo zimetolewa na Tume ya Madini Julai 18, 2025 kwa kipindi cha miaka saba ambazo ni PML Na.02977 katika mlima Kwaluhizo lenye ukubwa wa Hekta 4.96 na PML Na.02978 kwenye mlima Kwedihegwa lenye ukubwa wa Hekta 4.97.

No comments:
Post a Comment