MCHENGERWA : MIAKA 10 YA MAPINDUZI YA FIKRA, NAOMBA RIDHAA TUIJENGE RUFIJI YA NDOTO YETU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 4, 2025

MCHENGERWA : MIAKA 10 YA MAPINDUZI YA FIKRA, NAOMBA RIDHAA TUIJENGE RUFIJI YA NDOTO YETU



Na John Jayros


Mbunge anayetetea jimbo la Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema katika kipindi chote amekuwa mtumishi wa watu, mwanamapinduzi wa kweli anayejali maendeleo ya wananchi hivyo amewaomba wajumbe wampe ridhaa ya kuwaongoza ili kuendelea kuleta maendeleo.

Kauli hiyo ameitoa leo kwenye mkutano wa kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kesho kwenye kura za maoni kuwa mgombea wa jimbo hilo kwa mara ya tatu mfulizo.

Mkutano huo umefanyika Ikwiriri na uliohudhuriwa na maelfu ya wajumbe na wananchi waliokuja kusikuliza sera za watia nia wanne wa jimbo hilo ikiwa ni pamoja na Mhe. Mchengerwa anayetetea jimbo lake.

Amesema katika kipindi chake cha miaka 10 cha mapinduzi ya fikra na mageuzi makubwa ya maendeleo jimboni humo kumekuwa na mabadiliko kwenye kila sekta.

"Ndugu zangu katika safari hii sote tumejionea mapinduzi na mafanikio yaliyopatikana hivyo nawaombeni kwa kasi hii hii nipeni imani ili tuendelee kufanya maendeleo ya kweli ya jimbo letu". Amesisitiza Mhe. Mchengerwa

Ameongeza kuwa miaka 10 ya kazi, uaminifu, na uongozi thabiti imetosha kuonyesha mwelekeo wa wapi kwa kwenda.

Baadhi ya sekta ambazo amezitaja kuwa na mabadiliko na maendeleo makubwa ni pamoja na ongezeko kubwa la miundombinu ya sekta za elimu na afya , barabara na madaraja.


No comments:

Post a Comment