WMA WAONYA WANAOTUMIA VIPIMO BATILI KUWAPUNJA WAKULIMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 5, 2025

WMA WAONYA WANAOTUMIA VIPIMO BATILI KUWAPUNJA WAKULIMA



Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA


Wakala wa Vipimo (WMA) imewataka mawakala au wafanyabiashara wanaotaka kuwapunja wakulima na wananchi kwa kutumia vipimo batili kuacha mara moja kwani watachukuliwa hatua kali na Wakala hiyo pamoja na serikali kwa ujumla.

Hayo yameelezwa leo Agosti 05,2025 na Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Njombe Bw. Henry Msambila, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Wakala wa Vipimo, kwenye maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nane Nane) yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma.

"Wakala wa Vipimo tunaongozwa na Sheria ya vipimo sura namba 340, hivyo tukikubaini kama umefanya udanganyifu katika vipimo ikiwemo kosa la kuwapunja wakulima katika vipimo ambalo ni kosa la jinai tutakuchukulia hatua za kulingana na sheria hiyo ikiwemo faini ambazo zinaanzia laki moja hadi milioni ishirini," ameeleza Msambila

Aidha, amebainisha kuwa jukumu la msingi la Wakala wa Vipimo ni kumlinda mlaji kwa kuhakikisha matumizi ya vipimo sahihi katika biashara na huduma mbalimbali.

Pia amewakaribisha wananchi kutembelea banda hilo ili kujifunza zaidi kuhusu masuala ya vipimo na namna wanavyoweza kutambua vipimo sahihi dhidi ya batili, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuelimisha umma na kuimarisha uadilifu katika mizani ya biashara.

No comments:

Post a Comment