
Maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora leo Alhamisi Septemba 11, 2025 wamefurika kwa wingi uwanjani wakisubiri kuwasili kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan. Dkt. Samia anaendelea na ziara za kampeni za uchaguzi mkuu mkoani Tabora akitokea Singida, ambapo leo anatarajia kufanya mikutano katika wilaya za Uyui, Urambo na Kaliua na kunadi sera na ahadi za Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa wananchi wa mkoa huo.




No comments:
Post a Comment