UZINDUZI MKUBWA WA KAMPENI JIMBO LA MCHINGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, September 7, 2025

UZINDUZI MKUBWA WA KAMPENI JIMBO LA MCHINGA



Na Mwandishi Wetu, Rutamba, Lindi

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mchinga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Salma Rashid Kikwete, ambaye pia ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ameongoza uzinduzi mkubwa wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Uzinduzi huo umefanyika katika Kata ya Rutamba, kwenye viwanja vya Mahakama, ambapo Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, alikuwa mgeni rasmi.

Aidha, tukio hilo limepambwa na uwepo wa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Taifa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alihudhuria na kutoa baraka zake katika uzinduzi huo.

Katika hatua muhimu ya uzinduzi huo, Mhe. Salma Kikwete alipokea rasmi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 kutoka kwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa. Vilevile, Waziri Mkuu aliwakabidhi madiwani wote wa Jimbo la Mchinga nakala za Ilani hiyo, akiwataka kushirikiana kwa karibu na Mbunge ajaye katika utekelezaji wake.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Waziri Mkuu Majaliwa aliwahakikishia wananchi wa Mchinga kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi inatekelezwa ipasavyo, ili kuboresha maisha ya wananchi na maendeleo ya jimbo hilo.






No comments:

Post a Comment