NIDA YAPELEKWA KIDIGITALI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, December 29, 2025

NIDA YAPELEKWA KIDIGITALI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akibonyeza kitufe kuzindua namba maalumu (15274), itakayotumiwa na muombaji wa kitambulisho cha taifa, kufuatilia taarifa za maombi ya kitambulisho hicho.Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),James Kaji na wakwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Ofisi ya Zanzibar,Abdallah Mmanga.Tukio hilo limefanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akiangalia video fupi, inayofafanua matumizi ya namba ya kufuatilia maombi ya kitambulisho cha taifa baada ya kuizindua namba hiyo 15274 .Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),James Kaji na wakwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Ofisi ya Zanzibar,Abdallah Mmanga.Tukio hilo limefanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akizungumza wakati wa uzinduaji wa namba maalumu (15274), itakayotumiwa na muombaji wa kitambulisho cha taifa, kufuatilia taarifa za maombi ya kitambulisho hicho. Tukio hilo limefanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akikaribishwa na wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), alipowasili Makao Makuu ya Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuzindua namba maalumu (15274), itakayotumiwa na muombaji wa kitambulisho cha taifa.Tukio hilo limefanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),baada ya kuzindua namba maalumu (15274), itakayotumiwa na muombaji wa kitambulisho cha taifa, kufuatilia taarifa za maombi ya kitambulisho hicho.Watatu kulia waliokaa ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo,James Kaji na wakwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka, hiyo Ofisi ya Zanzibar,Abdallah Mmanga.Tukio hilo limefanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Na Mwandishi Wetu,DAR ES SALAAM


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amezindua namba maalumu, itakayotumiwa na wananchi kufuatilia kitambulisho cha taifa baada ya kuwasilisha maombi ya kitambulisho hicho, hali itakayopelekea wananchi kupata na kujua taarifa za maombi ya kitambulisho kwa kutumia namba maalumu hiyo.

Amezindua namba hiyo maalumu, leo jijini Dar es Salaam, ambapo amesema vitambulisho vingi vimezalishwa na tayari vimepelekwa sehemu husika, ikiwemo wilayani ambapo muombaji wa kitambulisho alijiandikishia na bado wahusika awajafuata kadi zao hali inayopelekea baadhi ya wananchi kukosa huduma mbalimbali huku akizitaja huduma za afya, mafao ya ustawi, usajili wa wanafunzi katika vyuo mbalimbali samabamba na maombi ya mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB).

“Hivi leo tunavyozungumza katika wilaya zetu zote nchini, viko vitambulisho vingi sana ambavyo havijachukuliwa na sababu kubwa inakua kwamba muombaji hajui kitambulisho chake kipo katika hatua gani, kupitia mfumo huu ambao ninauzindua utajibiwa na utaambiwa kama namba yako umepata ndani ya siku tano na kama ujapata ndani ya siku tano tangu ulipoomba ukitumia mfumo huu(15274) utajibiwa kwanini ujapata.”Amesema Waziri Simbachawene

Ameongeza pia serikali inafikiria kusitisha matumizi ya namba ya utambulisho (NIN) kwani watu wengi wameacha kwenda kuchukua vitambulisho vyao, ambavyo vimezalishwa kwa fedha nyingi ya kodi ya watanzania, hivyo wanapaswa kwenda kuchukua vitambulisho vyao na sio kutumia namba ya utambulisho kama kitambulisho.

Akizungumza katika uzinduzi huo,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),James Kaji amesema mamlaka imeendelea kushusha vitambulisho hadi ngazi ya kata lakini bado wananchi hawajavifuata vitambulisho na wameamua kuvipeleka wilayani na anaamini sasa kupitia mfumo huo mpya wa namba 15274 vitambulisho vitaendelea kufuatwa kwani mfumo huo umerahisisha zaidi taarifa za muombaji kupatikana mkononi kiganjani kwa kupitia simu ya mkononi.

No comments:

Post a Comment