RAIS MWINYI:UJENZI WA SKULI ZA GHOROFA NI SULUHISHO LA UHABA WA MADARASA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, December 27, 2025

RAIS MWINYI:UJENZI WA SKULI ZA GHOROFA NI SULUHISHO LA UHABA WA MADARASA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kutekeleza mkakati wa ujenzi wa skuli za ghorofa kama suluhisho la kudumu la changamoto ya uhaba wa madarasa na uendeshaji wa skuli kwa mfumo wa zamu ya asubuhi na mchana.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 27 Disemba 2025, alipoifungua Skuli Mpya ya Msingi ya Muungano iliyopo Kibanda Maiti, Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ameeleza kuwa Serikali inalenga kuongeza bajeti ya sekta ya elimu hadi kufikia Shilingi Trilioni Moja na kuifanya sekta hiyo kuwa sekta mama ya kipaumbele kwa maendeleo ya nchi.

Rais Dkt. Mwinyi amesema tayari Serikali imeshasaini mkataba na Benki ya CRDB wenye thamani ya Shilingi Bilioni 240 kwa ajili ya ujenzi wa skuli 29 za ghorofa, ambapo maandalizi ya ujenzi yameanza katika maeneo ya Fuoni Kibondeni, Jumbi na Chunga kwa Unguja, pamoja na Kiuyu Minungwini, Mchanga Mdogo na Micheweni kwa Pemba kupitia mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Rais Dkt. Mwinyi amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Nane tayari imejenga skuli 35 za ghorofa, hali iliyosaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani, ingawa bado yapo maeneo yenye changamoto hiyo hususan Mkoa wa Mjini Magharibi unaobeba zaidi ya nusu ya wakazi wa Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi amesema uimarishaji wa miundombinu ya elimu si suala la hiari bali ni wajibu wa Serikali ili kuhakikisha kila mtoto anapata mazingira bora ya kujifunzia, sambamba na kulinda misingi ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ya haki, usawa na upatikanaji wa huduma za msingi ikiwemo elimu.

Katika kuimarisha rasilimali watu, Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali imeajiri walimu wapya 1,741 katika mwaka 2024/2025, na tayari imeajiri walimu 492 katika mwaka wa fedha 2025/2026, huku lengo likiwa ni kuajiri walimu 1,500 pamoja na kuboresha maslahi yao.

Akitoa taarifa ya kitaalamu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Ndg. Khamis Abdalla Said, amesema Skuli ya Muungano ni ya ghorofa tatu yenye madarasa 42, maabara, chumba cha







No comments:

Post a Comment