WALIOPANGA KUCHOMA MATAIRI MKESHA WA MWAKA MPYA WAONYWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 31, 2025

WALIOPANGA KUCHOMA MATAIRI MKESHA WA MWAKA MPYA WAONYWA



Na Oscar Assenga, TANGA


MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian amewataka wananchi wa mkoa wa Tanga ambao wamepanga kutumia matairi kuchoma moto barabarani kama njia ya kusheherekea sikuuu ya mwaka mpya wasithubutu kufanya hivyo.

Dkt Batilda aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mkesha wa mwaka mpya ambao unatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga ambapo alisema kutokana huo ni uharibifu wa miundombinu ya barabara na hatari kwa Taifa.

Alisema kwamba ndio maana Ofisi ya Mkoa huo kwa kushirikiana na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga na Mbunge wa Jimbo la Tanga wameamua kufanya shughuli ya wana Tanga kwenye uwanja wa Burudani wa Uhuru Park.

Alisema kwamba kutakuwa na sanaa mbalimbali taarabu na miziki mbalimbali ikiwemo mashindano ya kupika maandazi ,vitumbua na watakaokuwa mabingwa wa kupika sambusa lakini watachoma samaki na mbuzi watu watakula bila gharama yoyote ili kuendeleza umoja,amani na ukarimu wa wana Tanga.

Aidha alisema kwamba baada ya hapo usiku watawasha mafataki watakayowashwa na wataalamu maalumu ya viwango maalumu hivyo kuliko kuchoma matairi waje kwenye uwanja wa uhuru ili kuona burudani mbalimbali ikiwemo mafataki.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wana Tanga kwenda uwanja wa Urithi ili kuweza kuomba dua kumshukuru Mungu kuuona mwaka na baada ya hapo mtu kurudi nyumbani ni eneo ambalo litakuwa salama.

No comments:

Post a Comment