WAZIRI MKUU Dkt. MWIGULU AAGIZA UJENZI WA BARABARA NJIA NNE TUNDUMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 17, 2025

WAZIRI MKUU Dkt. MWIGULU AAGIZA UJENZI WA BARABARA NJIA NNE TUNDUMA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameagiza ujenzi wa barabara njia nne eneo la Tunduma ili kupunguza msongamano.

Akizungumza katika ziara yake ya kukagua miundombinu mkoani Songwe Dkt. Mwigulu amezitaka taasisi zote za Serikali kushirikiana ili ujenzi huo uanze mara moja na hivyo kuufanya mpaka wa Tanzania na Zambia katika eneo la lango kuu la SADC kufanya kazi kwa tija na hivyo kuvutia wasafirishaji wengi.

" Miundombinu ikiwa bora huduma zikiimarishwa, amani na nidhami vikiwepo uchumi wa watu na taifa kwa ujumla utaimarika",
amesisitiza Dkt. Mwigulu.

Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema tayari Wakala wa Barabara nchini TANROADS umeanza maandalizi ya upanuzi huo katika eneo lenye urefu wa mita 700 kuwa njia nne.

Naibu Waziri Kasekenya amesema mkakati mwingine wa kupunguza msonamano ni kujenga mizani eneo la Iboya ili kupima magari yanayotokea mjini Tunduma na kuipunguzia msongamano mizani ya Mpemba ambayo itapima magari yatokayo Mbeya kwenda Tunduma.

Naibu Waziri Kasekenya amemhakikishia
Waziri Mkuu kuwa changamoto zilizojitokeza katika mizani ya Mpemba zimerekebishwa na sasa mizani hiyo inafanyakazi kwa ufanisi.

Waziri Mkuu yuko katika ziara ya kukagua miundombinu katika mikoa ya Songwe na Mbeya.


No comments:

Post a Comment