WAZIRI NANAUKA ATOA MAAGIZO KWA MAAFISA MAENDELEO YA VIJANA NCHINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 17, 2025

WAZIRI NANAUKA ATOA MAAGIZO KWA MAAFISA MAENDELEO YA VIJANA NCHINI




Na: Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana – Dodoma


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka ametoa maagizo manne (4) kwa Maafisa Maendeleo ya Vijana wa Mikoa na Halmashauri kwa lengo la kuboresha na kuimarisha ustawi wa vijana na Maendeleo yao nchini.

Aidha, Mhe. Nanauka amewataka maafisa hao, katika kutekeleza majukumu yao wahakikishe wanakuwa na takwimu sahihi za vijana waliopo katika maeneo yao na waweze kutambua changamoto zinazowakabili vijana na kutafuta ufumbuzi. Pili, kuwaunganisha vijana hao na programu na fursa zote za kitaifa zinazohusu ujuzi, ajira na uwezeshaji wa kiuchumi.

Vile vile, amewataka Maafisa Maendeleo ya Vijqna kuimarisha ushirikiano na wadau waliopo katika Mikoa na halmashauri zenu ili kuleta matokeo ya haraka na endelevu kwa vijana pamoja na kuzingatia uwajibikaji, uadilifu na matumizi sahihi ya rasilimali zinazotolewa kwa ajili ya vijana.

Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa Maendeleo ya vijana wa mikoa na halmashauri kilichofanyika ukumbi wa Hazina, leo Disemba 17, 2025, Jijini Dodoma.

Waziri Nanauka amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imechukua hatua za kimkakati za kuimarisha mifumo ya sera, sheria na utendaji kuhusu maendeleo ya vijana na hivyo kupelekea kuanzishwa Wizara yenye dhamana mahsusi ya Maendeleo ya Vijana chini ya Ofisi ya Rais.

Kwa upande mwengine, Waziri Nanauka ametoa rai kwa Maafisa Maendeleo ya vijana kuzingatia falsafa tatu (3) za wizara hiyo ambayo ni, Kasi ya kusikiliza na kutekeleza mawazo na ushauri wa vijana, Kuwafikia vijana walipo na kuwasikiliza na Kutumia teknolojia ili kwenda na kasi ya vijana.


No comments:

Post a Comment